SAJUKI KUZIKWA LEO MAANDALIZI YAENDELEA
MWILI
msanii nyota wa filamu, Juma Kilowoko “Sajuki” aliyefariki juzi
alfajiri, umeondolewa katika vyumba vya kuhifadhia maiti vya Hospital ya
Taifa, Muhimbili.
Na badala yake, mwili wa Sajuki sasa umekwenda kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha msikiti wa Shadhir (Masjid Shadhully) uliopo Kariakoo mtaa wa Sikukuu na Twiga.
Msanii Issa Mussa “Cloud” aliiambia mpekuzi kuwa lengo la kuhamisha mwili huo ni kujaribu kufanikisha taratibu zote kwenda na muda.
“Muhimbili process za kuchukua mwili ni ndefu na hata huduma zao za kuosha mwili wa marehemu ni ndefu pia kutokana na wingi wa maiti zinahofadhiwa na kuoshwa hospitalini hapo.
“Hivyo tumeona tuupeleke mwili Masjid Shadhully kwa vile hakuna msongamano kama wa Muhimbili” alisema Cloud.
Masjid Shadhully ndio msikiti
atakaoswaliwa Sajuki ambapo mwili wake utachukuliwa msikitini
hapo saa 4 asubuhi na kupelekwa nyumbani kwake Tabata na baadae
kurudishwa tena Masjid Shadhully kwa ajili ya kuswaliwa na kwenda
kuzikwa makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Ijumaa saa 7 za mchana.
No comments:
Post a Comment