MESSI MWANASOKA BORA WA DUNIA
|
Lionel
Messi akifurahi baada ya kupokea tuzo yake ya nne mfululizo ya Ballon
d'Or ya kwenye Ukumbi wa Convention Centre mjini Zurich Uswisi leo. |
|
Lionel Messi akiwa kwenye tuzo za FIFA leo |
|
Ronaldo, Iniesta na Messi wakiwa kwenye tuzo leo
|
|
Kikosi XI cha FIFA kilichotangazwa leo. Kutoka kushoto mstari wa nyuma Cristiano Ronaldo, Marcelo,
Sergio Ramos, Gerard Pique, Dani Alves, Iker Casillas. Mstari wa mbele
kutoka kushoto: Radamel Falcao, Lionel Messi, Andres Iniesta, Xavi
Hernandez na Xabi Alonso |
|
Fuleco, kikatuni cha fainali za
Kombe la Dunia 2014 za nchini Brazil kikimkumbatia mwanasoka bora wa
zamani Ronaldo stejini wakati wa sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or. |
|
Straika wa Real Madrid, Mreno
Cristiano Ronaldo na rafikiye wa kike Irina Shayk wakiingia kwenye
sherehe za tuzo za FIFA Ballon d'Or. NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi (25)
amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya soka kutwaa tuzo ya Ballon d'Or
ya Mwanasoka Bora wa Dunia kwa miaka minne mfululizo baada ya
kuwashinda wapinzani wake Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Andres
Iniesta wa Barcelona.
Muargentina huyo amekuwa mtu wa kwanza katika historia ya miaka 61 ya tuzo hiyo kuibeba mara nne mfululizo.
Johan
Cruyff (1971, 1973, 1974) na Marco Van Basten (1988, 1989, 1992) wa
Uholanzi, na Michel Platini wa Ufaransa walishinda tuzo ya Ballon d'Or
mara tatu.
Mwanadada Abby Wambach wa Marekani alishinda tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Kike, wakati tuzo ya kocha bora wa kiume ilienda kwa
Vicente Del Bosque wa timu ya taifa ya Hispania baada ya kuwashinda,
Jose Mourinho wa Real Madrid ambaye alishasema mapema kwamba
hatahudhuria sherehe hizo nchini Uswisi na Pep Guardiola.
Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la Mwaka ilienda kwa winga wa Fenerbahce, raia wa Slovakia, Miroslav Stoch ambaye alifunga goli lake kwa kuunganisha moja kwa moja bila ya kutua chini mpira wa kona uliomfikia akiwa nje ya boksi. Stoch aliwaangusha Radamel Falcao aliyefunga goli la 'tik-taka' na Neymar aliyefunga goli katika mazingira magumu.
Kikosi cha wachezaji bora "First Eleven"
wa dunia chote kimeundwa na nyota wanaocheza katika Ligi Kuu ya
Hispania, huku Radamel Falcao pekee akitokea nje ya Barcelona na Real
Madrid.
Real Madrid na Barcelona zimetoa wachezaji watano kila moja.
Kikosi Bora cha Dunia XI cha FIFA kilichotangazwa leo ni:
Kipa Iker Casillas
Mabeki Dani Alves, Marcelo, Sergio Ramos na Gerard Pique
Viungo Xabi Alonso, Xavi Hernandez na Andres Iniesta
Mastraika Cristiano Ronaldo, Radamel Falcao na Lionel Messi |
|
No comments:
Post a Comment