AMINA NA LINA TENA KUFANYA SHOW 'USIKU WA MTIMA WANGU'
|
Baada ya kufanya show kali katika fainali za BSS mwishoni mwa mwaka
jana na kuzua mjadala kama wapenzi hawa wa zamani wamerudiana, wasanii
wa THT Amini na Linah wanatarajia kufanya show nyingine pamoja huko
Kigamboni, Dar es Salaam waliyoipa jina la ‘Usiku wa Mtima Wangu’.
Show hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Club Kakala siku ya
Jumamosi ya January 5 ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 6,000 tu.
Wasanii hao kwa sasa wana wimbo mpya uitwao Mtima Wangu unaofanya vizuri kwenye vituo vya radio. |
No comments:
Post a Comment