TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, September 30, 2015

Hizi ni safari ndefu zaidi za Ndege Duniani, unakaa mpaka saa 17 angani mtu wangu.. (+Pichaz)

Unaweza ukaona safari ya kutoka Mwanza mpaka Dar es Salaam ni ndefu kwa sababu unatumia kati ya saa 12 mpaka 16 ndani ya basi, lakini kwa Usafiri wa Ndege ni kama saa moja tu hivi unakuwa umemaliza safari !!
Sasa hizo saa za kukaa kwenye basi safari ya Mwanza-Dar kuna watu wanazitumia wakiwa angani kwenye Ndege… Nimezipata Rekodi Mitandaoni, zinaonesha safari kumi za Ndege ambazo wasafiri wanatumia muda mwingi zaidi hewani kwenye safari moja.
1.Dubai Mpaka Panama– Hii ni Safari ambayo inachukua saa 17 na dakika 35 angani… yani Ndege ikiruka Dubai hakuna sehemu inatua mpaka ifike Panama. Hii ndio safari ndefu zaidi kwa sasa ambayo inafanywa na Ndege za Emirates… umbali toka Dubai mpaka Panama ni Kilometa 13, 820.
emirates (1)2. Dallas mpaka Sydney- Unaambiwa umbali toka Dallas Marekani mpaka Sydney Australia ni Kilometa 13,804. Hiyo ni safari ambayo inachukua saa 17 kwa Ndege za Qantas.
3. Atlanta mpaka Johannesburg– Hapo kuna umbali wa Kilometa 13,580.. safari hii inakamilika kwa Ndege za Shirika la Delta kukaa angani kwa saa 16 na Dakika 55 ambazo ni kama saa 17 hivi mwanzo mpaka mwisho wa safari.
60966325
4. Los Angeles mpaka Dubai– Kama kuna wakati unawaza kufanya safari kati ya hayo Majiji mawili, basi utambue kabisa kwamba umbali wake ni Kilometa 13,420.. na Ndege inatumia saa 16 na Dakika 30. Hii sio safari fupi hata kidogo mtu wangu !!
5. Los Angeles mpaka Jeddah– Shirika la Ndege la Saudi Arabia ndio ambao wamekamata hii njia, unaambiwa umbali toka Los Angeles Marekani mpaka Jeddah Saudi Arabia inakuchukua saa 17 pia kuimaliza hiyo safari yenye umbali wa Kilometa 13,409.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
Picha ya muonekano wa juu wa Jeddah Airport mpya, Saudi Arabia.
6. Los Angeles mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji miwili ni Kilometa 13,500.. sio safari ndogo aisee, Ndege za Etihad zinakamilisha hiyo safari kwa saa 16 na Dakika 50 mwanzo mwisho.
7. Houston mpaka Dubai– Kilometa 13,145 zimetajwa kwamba ndio umbali kati ya Miji hiyo miwili, safari yake mwanzo mpaka mwisho kwa Ndege inachukua muda wa saa 16 na Dakika 10… Ndege za Emirates zinahusika pia kusafirisha watu kati ya Miji hii miwili.
8. San Francisco mpaka Abu Dhabi– Umbali kati ya hiyo Miji ni Kilometa 13,130.. na safari yake inachukua saa 16 kukamilika.
9. Dallas mpaka Hong Kong– Hapo unazungumzia Marekani na China, umbali wake ni Kilometa 13,700 na umbali huo kwa safari ya Ndege inachukua saa 16 na Dakika 15… Ndege za American Airlines zimeunganisha hii Miji miwili kwa Ndege za moja kwa moja.
American_Airlines_Boeing_777-200ER_N775AN_PVG_2013-5-21
10. San Francisco mpaka Dubai– Hii nayo imo kwenye list ya safari ndefu za Ndege, umbali wake ni Kilometa 13,040… Ndege za Emirates zimeunganisha hii Miji pia kwa safari ya Ndege ya moja kwa moja. Safari yote inakamilika ndani ya saa 16 na Dakika 40.

No comments:

Post a Comment