Mtoto wa mchezaji bora wa dunia kutokea Brazil amejiunga na klabu hii ya Ureno
         
Mtoto wa mchezaji wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Rivaldinho Rivaldo ambaye anafuata nyayo za baba yake Rivaldo katika soka, amesajiliwa na klabu ya Boavista ya Ureno akitokea klabu ya Mogi Mirim ya kwao Brazil. Hivyo hiyo inakuwa mwanzo wa safari yake ya kusaka mafanikio kama aliyoyapata baba yake Ulaya.
Rivaldinho ambaye ana umri wa miaka 20 amejiunga na klabu ya Boavista
 kwa mkataba wa miaka mitatu na kuhama katika klabu ambayo baba yake 
mzazi ni Rais, hiyo itamfanya kukua na kukomaa kisoka kwani ataanza 
kuishi mbali na uangalizi wa baba yake.
Mchezaji huyo ambaye amepata umaarufu 
kutokana na ukubwa wa jina la baba yake, ni kawaida kuingia katika 
headlines kila mara anapofunga goli, ameichezea klabu ya Mogi Mirim jumla ya mechi 44 na kufunga goli 10. Rivaldinho ili aweze kufikia rekodi za baba yake inabidi ajitume kwani hadi sasa hajawahi cheza katika timu ya taifa ya Brazil hata ya vijana.


No comments:
Post a Comment