Mwaka mmoja tangu kupotea wanafunzi Mexico, msimamo wa wazazi ni huu..Serikali je?
         
Tarehe kama ya leo Mexico iliingia 
kwenye headlines baada ya kuwepo na taarifa ya kupotea kwa wanafunzi 43 
katika mji wa Iguala Kusini mwa nchi hiyo.

Pamoja na kuwepo utata wa kupotea 
kwa wanafunzi hao huku ndugu wa wanafunzi hao wakigoma kupokea taarifa 
ya Serikali iliyotolewa baada ya uchunguzi uliodai wanafunzi hao 
walitekwa na kuuawa na kundi la kigaidi.
Ripoti hiyo haijakataliwa tu na ndugu wa wanafunzi hao, bali pia 
ripoti kutoka kwa kundi la wataalamu wa uchunguzi hivi karibuni ilihoji 
uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.Ndugu wa wanafunzi hao wamesisitiza kuwa hawataacha kuandamana hadi pale watakapojua ukweli juu ya ndugu zao hao.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.

No comments:
Post a Comment