David Beckham anatarajiwa kucheza movie ya James Bond 007
         
Staa wa zamani wa klabu za Real Madrid, Man United, LA Galaxy na timu ya taifa ya Uingereza David Beckham anatarajiwa kuonekana katika movie. Beckham mwenye umri wa miaka 40, imeripotiwa kwa mujibu wa mtandao wa mirror.co.uk, unamtaja David Beckham kucheza katika movie ya James Bond.
Beckham anatajwa kuchukua nafasi ya Daniel Craig ambaye mkataba wake unakaribia kumalizika, Beckham ambaye
 ni baba wa watoto wa nne amekiri kuwa aliwahi kufikiria kucheza movie 
baada ya mashabiki kushauri hilo . Hata hivyo taarifa hizi sio ngeni kwa
 mashabiki wa Beckham kwani ameshawahi kukiri kushawishika katika masuala ya movie.


No comments:
Post a Comment