Ndege ilivyoshika moto wakati inajiandaa kupaa Marekani
Kama hii dharura ingetokea wakiwa
katikati ya safari basi vyombo vya Habari Duniani vingekuwa na stori
tofauti kabisa… Ndege ya Shirika la British Airways ilikuwa tayari kwa
ajili ya safari kutoka Uwanja wa Ndege Las Vegas Marekani, ndani
kulikuwa na abiria 159 pamoja na wahudumu wa Ndege 13.
Ajali hiyo ilitokea ghafla ambapo injini
ya kushoto ilishika moto wakati ndege hiyo tayari ilikuwa kwenye njia
ya kuruka… ikabidi safari iishie hapo na abiria wote watoke ndani ya
Ndege kwa dharura.
Majeruhi ni wachache ambao walipata majeraha madogo madogo lakini hakuna taarifa ya mtu yoyote kufariki.
Muda mfupi baadae Rubani mmoja wa Ndege
hiyo aliwaambia abiria hao kwamba ana uzoefu na kazi ya Urubani kwa muda
mrefu lakini hakuwahi kupata tatizo la aina hiyo katika kazi yake, na
chanzo cha moto huo ilikuwa ni tatizo la kiufundi kwenye injini ya Ndege
hiyo.
No comments:
Post a Comment