TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, September 9, 2015

Hizi ni taarifa nyingine mbaya kwa Emmanuel Adebayor katika timu yake ya taifa

Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor bado yupo katika wakati mgumu katika maisha yake ya soka. Adebayor jina lake halipo katika list ya wachezaji watakaoshiriki michuano ya Europa League.
Baada ya siku kadhaa kupita toka taarifa za jina lake kutowekwa katika list ya kikosi kitakachoshiriki Europa League, Adebayor analaumiwa na kocha wa timu ya taifa ya Togo kwa kukosa uzalendo na kuwa hapendi kuona timu hiyo ikifuzu kucheza michuano ya AFCON 2017 Gabon.
REU_1981974
Kocha wa Togo Tom Saintfiet hakumuita kikosini Adebayor baada ya wiki iliyopita kumuita kikosini lakini hakutokea kujiunga na kikosi cha timu yake ya taifa.
“Kwangu mimi hili suala lipo wazi Adebayor ni mchezaji ambaye haitaji kuichezea nchi yake na hataki kuona tukifuzu AFCON, alikubali kuja kucheza mechi ya Liberia lakini Djibout hakutaka kuja kucheza , sasa sula la kuamua ni mechi ipi ya kucheza sio la mchezaji ni la kocha”>>> Tom Saintfiet
“Kama huko katika mahusiano na msichana ambaye hataki kuonyesha ushirikiano katika mahusiano yenu, utalazimika kutafuta mwingine ambaye ana ushirikiano na wewe”>>> Tom SaintfietBurkina-Faso-v-Togo-2013-Africa-Cup-of-Nations-Quarter-Final
Emmanuel Adebayor ambaye hana nafasi kwa sasa katika kikosi cha Tottenham Hotspur ya Uingereza, kitu kilichopelekea namba yake ya jezi kupewa Harry Kane, hivyo Tom Saintfiet kaamua kumuacha katika timu ya taifa, baada ya kuchagua mechi anazotaka kucheza. kwa sasa Adebayor anafanya mazoezi na timu ya watoto.

No comments:

Post a Comment