Jamaa kakosea kutuma ujumbe ukaenda kwa Polisi ili apatiwe dawa za kulevya…kilichofuata?
         
William Lamberson raia wa Florida,Marekani amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kutuma ujumbe wa maneno kwa Polisi akidhani ni rafiki yake.
Ujumbe huo ulilenga kutaka apatiwe dawa za
 kulevya kutoka kwa rafiki yake huyo ambaye walikuwa wakishirikiana 
katika biashara hiyo lakini alikosea na kujikuta ukienda kwa  Brian Bergen ambaye ni kiongozi wa Polisi.
Polisi walianza kufanya uchunguzi wao na 
kugundua Lamberson anajihusisha na uuzaji wa dawa hizo hivyo baada ya 
uchunguzi aliwekwa ndani na kufunguliwa mashtaka ya kujihusiha na 
biashara hiyo haramu.

No comments:
Post a Comment