Hii ni rekodi inayoipeleka Juventus kinyonge katika mechi yake dhidi ya Man City…(+Pichaz)
Klabu ya Juventus ya Italia tayari imewasili jijini Manchester kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya klabu ya Manchester City katika mechi yake ya kwanza ya Kundi D. Licha ya kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliyomalizika, klabu ya Juventus haijaanza vizuri katika mechi zake 3 za Ligi Kuu Italia.
Juventus wamecheza mechi tatu hadi sasa za Serie A, mechi dhidi ya Udinese na kupoteza kwa 1-0 wakiwa nyumbani, baadae kufutia kwa kipigo cha pili cha goli 2-0 kutoka kwa Roma kabla ya mechi yake ya tatu kucheza na klabu ya Chievo na kuambulia point moja baada ya kutoka sare ya goli 1-1.
Licha ya kuwa na mwanzo mbaya wa Ligi Kuu ukilinganisha na wapinzani wao Man City ambao wanaonekana kuwa vizuri kwa kufanya vizuri katika mechi zao 5 za Ligi Kuu Uingereza na kuongoza Ligi hiyo, kocha wa Juventus Massimiliano Allegri tumaini pekee linalombeba na kuipa presha Man City ni rekodi yake ya kufanya vizuri msimu uliyopita katika Ligi ya Mabingwa.
No comments:
Post a Comment