Sababu ya kushindwa kusajiliwa De Gea Real Madrid na maamuzi ya klabu hiyo kwa FIFA viko hapa…
Golikipa wa kimataifa wa Hispania ambaye anaichezea klabu ya Manchester United David De Gea, alikuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania, hivyo kila kitu kilikuwa kimesha kuwa sawa ikiwemo maslahi binafsi ya mchezaji.
De Gea ambaye aliripotiwa usiku wa August 31 kuwa karibu na kujiunga na Real Madrid timu aliyokuwa akihusishwa kujiunga nayo tokea zamani, mpango wa De Gea kujiunga na timu hiyo ulikwama baada ya viongozi wa Man United kuchelewa kutuma mikataba katika klabu ya Real Madrid, hivyo walituma dakika moja baada ya dirisha la usajili kufungwa.
Tatizo la kuchelewa kwa documents za mikataba hiyo ni mfumo wa usajili wa FIFA ndio umefanya documents kutoka klabu ya Man United kuchelewa kufika kwa Real Madrid, kutokana na Real Madrid kuwa na ushaidi wa hizo documents watakata rufaa FIFA ili wapewe nafasi ya kumsajili De Gea nje ya muda wa usajili kwani mfumo wa FIFA ndio uliochelewesha usajili huo.
Klabu ya Real Madrid ya Hispania na Man United walikuwa wamekubaliana kuuziana golikipa huyo kwa ada ya pound milioni 29 pamoja na kupewa golikipa Keylor Navas, kama rufaa yao haitashinda watalazimika kusubiri hadi dirisha dogo mwezi January, dirisha la usajili kwa upande wa Hispania na Ufaransa tayari yashafungwa.
No comments:
Post a Comment