Umewahi kuona kisiwa kinahama? Hiki hapa, unaweza kuhisi ni Boti au Meli ..!! (+Pichaz)

Ubunifu wa binadamu na maendeleo ya
Teknolojia ni vitu ambavyo huwa vinatuletea mambo mapya kila siku,
hakuna mtu asiyependa kusifiwa baada ya kufanya kazi nzuri.. ubunifu wa
hiki kisiwa ni kazi nzuri ambayo tayari pongezi zimeanza kuwafikiwa
wabunifu walioona kuna umuhimu kuwa na kitu kama hiki cha kuvutia.
Tunajivunia uzuri wa Zanzibar yetu, huo
ni uzuri kwenye kisiwa cha asili kabisa.. taarifa ikufikie kwamba wapo
waliowaza kutengeneza kisiwa kinachohama kwa kutembea juu ya maji kama
ilivyo meli au Boti.
Najua kwamba Dunia inavitambua pia visiwa vilivyotengenezwa na binadamu ikiwepo Palm Island, ambacho kiko Dubai… lakini Dunia inatambulishwa pia kwenye Kisiwa ambacho kimebuniwa na wataalam wa Kampuni ya Migaloo ambao wanadili sana na kutengeneza Boti za kifahari.
Ubunifu huu utasogezwa kwenye Maonesho maalum ya Monaco Yatch Show
na tayari watu wenye pesa zao wameonekana kuvutiwa sana na hii kitu,
kwa hiyo tayari ni biashara ambayo inatarajia wateja wa nguvu kabisa any
time kuanzia sasahivi !!

Ukiangalia nje mpaka ndani Kisiwa hiki
kinavutia, na kina mahitaji yote muhimu kwa mtu anayehitaji kuishi ndani
yake, kwenye vilivyomo unaambiwa mpaka Beach za nguvu kabisa zipo ndani
!!


Hii
ni Beach ambayo iko kwenye kisiwa hicho cha kisasa kabisa, na ardhi
ambayo iko kwenye kisiwa ni kama ambayp iko kwenye maeneo yenye hali ya
kitropiki.


Juu kwa juu mtu wangu, hapo kuna Beach ya nguvu kisiwani, Bustani na miti.. vyote vinaongeza uzuri wa Kisiwa hiki.

Ndani
kunavutia mtu wangu, yani huku ndani unaambiwa kuna Beach nyingine na
mazingira poa kabisa ya kujienjoy !! Ukiingia mpaka unajisahau kwamba
uko kwenye kisiwa kinachoelea.
Ubunifu huo wa nguvu huu hapa pia kwenye video mtu wa nguvu, teknolojia ina mazuri yake ya kuvutia kila siku yani !!
No comments:
Post a Comment