Jorge Mendes ndiye jamaa anayevuna pesa nyingi katika kipindi cha usajili
Ikiwa ni siku moja toka dirisha la usajili lifungwe barani Ulaya,
kila klabu inajiandaa kupiga mahesabu ni kiasi gani cha fedha imetumia
kwa ajili ya kufanya usajili. Lakini wakati vilabu vikipiga hesabu ya
kiasi gani imetoa na kuingiza wakati wa usajili, kuna mtu anaitwa Jorge Mendes yeye wakati huu, huwa anapiga hesabu ya kiasi alichoingiza.
Jorge Mendes
ni wakala maarufu ambaye anafanya shughuli hiyo kwa wachezaji kadhaa,
huwa anatanguliza maslahi mbele kuliko kitu kingine chochote. Kati ya
mwaka 2001 hadi 2010 amehusika kwa asilimia 68 katika kila usajili wa
kuuza wachezaji kutoka vilabu vya Benfica,Porto na Sporting Lisbon za Ureno.
Mreno huyu kwa hivi siku za karibuni amekuwa ana husika kwa nafasi kubwa katika usajili unaofanywa na vilabu vya Atletico Madrid, Deportivo La Coruna, Monaco na Valencia. Huyu ndiye wakala ambaye mara nyingi ufaidika katika uhamisho wa masaa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Haikuwa safari rahisi kwa Jorge Mendes kuwa wakala mkubwa wa wachezaji wa kubwa, safari ilianza mwaka 1996 kwa mteja wake wa kwanza Nuno walipo kutana katika Bar ya Guimaraes na kufanikisha uhamisho wa Nuno kwenda katika klabu ya Deportivo . Mendes ni wakala wa Cristiano Ronaldo na wachezaji wengine wengi.
Diego Costa ni moja kati ya wateja wa Mendes hiki ni kitu alichowahi kufanyiwa na Mendes katika masuala ya usajili.
“Jorge
aliniambia natakiwa kupanda ndege na kwenda Madrid lakini nilikuwa sijui
nini kinaendelea nilivyofika aliniambia alikuwa anasaini Atletico
Madrid, baadae akaniambia kuwa tulikuwa katika nyumba ya mkurugenzi wa
michezo wa Atletico Madrid Jesús García Pitcarch nilikuwa simjui hata
kidogo”>>> Diego Costa
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jorge Mendes ndiye wakala aliyepewa zawadi ya kisiwa na Cristiano Ronaldo katika harusi yake, kupitia biashara hiyo katika kipindi cha miaka 20, Mendes anatajwa kuingiza kiasi cha pound bilion 1 na anatajwa kama wakala ambaye mipango yake ya uhamisho mingi huwa inafanikiwa
No comments:
Post a Comment