Hii ndio adhabu aliyoipata Juma Nyoso baada ya kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji John Bocco
Jioni ya September 27 ilikuwa ni siku
ambayo wadau wengi wa soka walikuwa wakijadili kuhusiana na tukio la
kidhalilishaji, lilitokea katika mechi ya Azam FC dhidi ya Mbeya City, mechi ambayo ilipigwa katika uwanja wa nyumbani wa Azam FC Azam Complex Mbande Chamazi.
Tukio lililotokea katika mechi hiyo ambalo kila mpenda soka Tanzania hakulipenda ni beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City Juma Nyoso kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco, baada ya tukio kufanyika kila mtu aliongea lake ila Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi alithibitisha kupitia account yake rasmi ya twitter kuwa sheria kali zitachukuliwa dhidi ya Juma Nyoso.
Taarifa mpya kutoka katika kamati ya uendeshaji wa Ligi, zinaeleza kukaa chini na kupitia kosa la Juma Nyoso
na kuamua kumpa adhabu ya kumfungia kucheza soka katika kipindi cha
miaka miwili pamoja na faini ya milioni 2. Kamati hiyo imefikia maamuzi
hayo kutokana na Juma Nyoso kuwa mkosefu sugu wa kitendo hicho cha kidhalilishaji katika mchezo wa soka.
Hii sio mara ya kwanza kwa Juma Nyoso
kufanya tukio kama hilo, kwani alishawahi kufungiwa mechi nane kwa
tukio kama hilo, baada ya kumfanyia mshambuliaji wa zamani wa Simba Elias Maguli, hayo ndio matukio ambayo Nyoso amewahi kukamatwa na kuadhibiwa nayo ila September 28 beki wa zamani wa Yanga Amir Maftah amekiri kuwahi kufanyiwa kitendo hicho na Juma Nyoso na yeye kupatwa na hasira na kumpiga kichwa katika mechi dhidi ya Simba, tukio ambalo lilisababisha Amir Maftah kuonyeshwa kadi nyekundu.
No comments:
Post a Comment