Rais MUGABE karudi kwenye headlines baada ya maamuzi haya kutoka kwa wapinzani…
         
Mwezi uliopita Rais wa Zimbabwe 
Robert Mugabe alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya wabunge wa vyama 
vya upinzani kumzomea wakati akitoa hotuba wakimshutumu kushindwa 
kuiongoza vyema nchi yao.
Headlines zimerudi tena kwa Rais 
huyo baada ya jana Bunge hilo kuahirisha matangazo ya LIVE ya redio na 
Televisheni ya hotuba ya Mugabe kutoka kwa vyama vya upinzania 
wakitishia kuvuruga hotuba hiyo kwa mara nyingine.
Wapinzani hao wamekua wakimlaumu 
rais wao kuendelea kung’ang’ania madarakani wakati uchumi wa nchi hiyo 
ukizidi kudidimia kila siku.
Rais Mugabe ambaye sasa ametimiza miaka 91 amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.Spika wa Bunge Jacob Mudenda amevionya vyama hivyo kuacha mara moja vurugu hizo lakini juhudi zake ziligonga mwamba na kusababisha vituo vya matangazo kusitisha kurusha matangazo hayo LIVE.
No comments:
Post a Comment