TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, September 11, 2015

Hizi ni dalili za David de Gea kuongeza mkataba Manchester United? wakala na familia yake waongeza uvumi

Joges Mendes ni wakala wa wachezaji soka lakini ndiye mtu anayetajwa kuwa na nguvu kubwa katika mpira wa miguu, hususani katika masuala ya uhamisho wa wachezaji kutoka timu moja kwenda timu nyingine. Wakala huyo ambaye ni wakala wa David de Gea, amewasili katika uwanja wa mazoezi wa Man United.
Wakala huyo alipigwa picha akiwasili katika uwanja wa mazoezi wa Man United Carrington, akiwa katika gari la watu wanne, Joges Mendes anawasili Man United ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka uhamisho wa mteja wake David de Gea wa kujiunga Real Madrid ushindikane kutoka kuchelewa kwa nyaraka za mikataba.
2C25FAA800000578-0-image-a-2_1441892968046
Ujio wa Joges Mendes katika jiji la Manchester hususani kuwasili katika uwanja wa mazoezi wa Man United kunaongeza uvumi wa David de Gea kuongeza mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho, kwani kipa huyo mkataba wake na Man United umesalia miezi kadhaa kumalizika kitu kinacholeta hofu kwa viongozi wa Man United kuwa, huenda akajiunga na Real Madrid baada ya mkataba wake kumalizika.
2BEAD4BC00000578-0-image-a-5_1441893047468
Ripoti kutoka katika vyombo vya habari vya Uingereza inaeleza kuwa familia na wakala wa David de Gea wamewasili Manchester September 10, huenda kipa huyo akisaini mkataba wa pound milioni 4 kwa mwaka na kuendelea kuitumikia Manchester United.

No comments:

Post a Comment