Hadi July 2014 hawa ndio mastaa 12 wa soka wanaotajwa kuwa wakali wa mitindo (Pichaz)
Hadi July 2014 mtandao wa artbecomesyou.com ulikuwa unawataja mastaa kadhaa wa soka kuwa ndio wakali wa style
za mavazi. Licha ya watu wengi kuwa wanaamini kuwa ukiwa na fedha,
utakuwa unavaa sana pamba na mkali wa mitindo, ndio ni kweli ili
upendeze lazima uingie gharama, unaweza vaa vitu vya gharama lakini
usipendeze kutokana na mpangilio wako, ila mastaa hawa ndio wanaotajwa
kuwa wakali katika masuala ya mavazi.
- David Beckham jamaa ana nyota ya kupendwa kutokana na muonekano wake na ustaa wake kapewa nafasi ya kwanza katika masuala ya kupangilia pamba na mitindo.
2. Samuel Eto’o uhodari wake haukuishia uwanjani tu hata katika masuala ya mitindo huwa ni mkali pia.
3. Daniel Sturridge huyu ni mkali wakuzifumania nyavu katika soka, kwa suala la mitindo tu yupo vizuri.
4. Raul Meireles staa kutokea Ureno
anatajwa kama mgonjwa wa masuala ya mitindo na mavazi japo mavazi yake
mingine du!! watu hushangaa ila naye yumo katika hii list.
5. Cristiano Ronaldo tumezoea kumuona akiwa katika headlines kutokana na jina lake, kwa mavazi tu yupo vizuri.
6. Didier Drogba style yake ya nywele pekee inatosha kumjua kuwa ni mtu wa masuala ya kwenda na wakati (Fashion)
7. Thierry Henry heshima yake haijaishia katika klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, hata katika ulimwengu wa Fashion wanamtambua.
8. Mario Gomez anatajwa kuwa na muonekano wa models wa fashion hivyo jina lake na muonekano wake humfanya apate mikataba ya kutangaza nguo wakati mwingine.
9. Sergio Ramos yupo sawa na mchezaji mwenzie wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, wote ni wakali katika masuala ya fashion.
10. Djibril Cisse ni staa kutokea Ufaransa, kwanza ana muonekano wa kipekee tofauti na wengine kuanzia style ya nywele, ndevu hadi mavazi.
11. Andrea Pirlo anatajwa kuwa akivaa mavazi mengine tofauti na mavazi ya soka unaweza usimtambue kwa muonekano wake aliyo nao.
12. Keisuke Honda mjapan pekee aliye bahatika kuwa katika hii list ya wakali wa style kwa muonekano na mavazi .
No comments:
Post a Comment