TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, September 14, 2015

Licha ya ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Liverpool Louis van Gaal hakiamini kikosi chake

Kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye amekiongoza kikosi chake kupata ushindi mnono katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza September 13 dhidi ya Liverpool ameshindwa kuthibitisha ubora wa kikosi chake wa kuzifunga timu zingine katika michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya.
Van Gaal alishindwa kutoa jibu la kuwa kikosi chake ni bora na kitafanya vizuri katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya katika mchezo wa kundi B dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. Man United ni moja kati ya vilabu vya Uingereza vitavyocheza mechi za Ligi ya mabingwa Ulaya September 15.
Louis van Gaal
“Msimu uliyomalizika wa Ligi Kuu tulishika nafasi ya nne na kufuzu kucheza Ligi ya mabingwa, hilo ndio lilikuwa lengo letu, lakini sasa tunalazimika kucheza kwa kiwango cha juu lakini sina uhakika na hilo tusubiri tuone, nafikiri Ligi ya mabingwa ni mashindano magumu kuliko Ligi Kuu, lakini huenda isiwe kama ninavyofikiria”>>> Van Gaal

No comments:

Post a Comment