Utatamani kuyaona mazuri ya Nigeria 2016? Na huu mjengo kama wa Marekani utakuwepo !! (Pichaz)
         
Kwenye list ya nchi ambazo zina uchumi 
mzuri zaidi Africa, Nigeria imo… YES, yani hata ukizitaja tatu bora nayo
 imo… Nigeria imetajwa kama nchi yenye uchumi mzuri mwaka 2015 na 
yenyewe inashika nafasi ya tatu, wakati ya kwanza ni South Africa na ya 
pili ni Egypt !!
Lakini kama unakumbuka vizuri, September
 11 kila mwaka nchi ya Marekani ina kumbukumbu ya tukio la shambulio la 
Kigaidi lililotokea New York, kwenye Jengo kubwa la Biashara la Kimataifa, World Trade Center mwaka 2001.

Baada ya kulipuliwa kwa Majengo ya kwanza, Marekani walijenga upya eneo hilo na huu ndio mwonekano wa sasahivi Majengo ya One World Trade Center, New York Marekani.
Sasa jina la World Trade Center linakuja Africa,
 Mjengo unashushwa rasmi kabisa katikati ya Jiji la Abuja Nigeria… kitu 
kitakuwa ni cha kisasa na ndani yake kutakuwa na  vyumba vya Biashara 
pamoja na apartments ambazo watapangishwa watu na watakuwa wanaishi kama
 home tu yani !!

Moja ya Majengo ya World Trade Center ya Nigeria, Ujenzi umefikia hapa tayari.
Unaambiwa mpaka hiki kitu kikikamilika 
kitakuwa kimeweka Rekodi ya kuwa Jengo kubwa zaidi Afrika Magharibi 
ambalo ndani yake kuna shughuli za aina nyingi zinafanyika.

Ufunguzi wa Jengo hilo utafanyika mwaka 2016 ambapo awamu ya kwanza ya Ujenzi itakuwa imekamilika.





No comments:
Post a Comment