Mtoto wa Beckham amelikataa soka? Haya ndio maneno yaliyomuumiza baba yake
         
David Robert Joseph Beckham
 ni staa wa Soka ambaye kastaafu Soka na kuacha Rekodi kubwa na nzuri 
zinazoheshimika Duniani, yako maneno kwamba maji hufuata mkondo, mtoto 
wa Beckham na Soka la Baba yake je?
Stori ni vice versa, David Beckham kathibitIsha kwamba mtoto wake na Mchezo wa Mpira wa Miguu hata haviendani >>> “Mwanangu
 mmoja aliniambia kwamba haoni kama atakuja kuwa Mchezaji wa Mpira wa 
Miguu kwenye maisha yake, ilinivunja moyo kwa upande mwingine“- David Beckham.
Kwenye sentensi nyingine Beckham anasema mtoto wake ana hofu kwamba wapo watakaolinganisha kiwango chake na baba yake >>> “Kila nikiingia uwanjani najua watu wanasema ‘yule ni mtoto wa Beckham’, nisipokuwa na kiwango kizuri kama wewe hata haipendezi“- David Beckham.


No comments:
Post a Comment