Wahamiaji:Muungano wa Ulaya wapingwa
Waandamanaji wakipinga vifo vya wahamiaji wanaovuka bahari ya shamu kwenda Ulaya
Makundi
ya kupigania haki za kibinadamu yamesema kuwa mikakati ilioafikiwa na
muungano wa ulaya kuzuia idadi kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka
hadi Ulaya kutoka Afrika sio ufumbuzi wa tatizo hilo.
Katika
kikao cha dharura kilichofanyika mjini Brussels siku ya alhamisi,
Viongozi wa Ulaya walikubaliana kuongeza msaada wao mara tatu ili
kuimarisha usakaji na uokozi wa wahamiaji katika bahari ya shamu.
Pia waliidhinisha mikakati ya kukamata na kuharibu vyombo vinavyotumiwa kuwasafirisha wahamiaji hao.
Lakini
Shirika la Human Rights Watch pamoja na lile la kuwasaidia watoto la
Save the Children, yanasema kuwa EU inafaa kuongeza juhudi zake katika
uokoaji badala ya kullinda mipaka yake.
Mkutano huo uliitishwa baada ya zaidi ya watu 800 kuuawa wikendi iliopita baada ya boti yao kuzama.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment