Gabon mwenyeji wa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika 2017
Shabiki wa timu ya soka ya Gabonwakati wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2012.
Na RFI
Gabon
imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika katika mwaka
2017, shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza Jumatano Aprili 8
mwaka 2015 katika mji mkuu wa Misri, Cairo.
Gabon ni
moja ya nchi tatu ziliyokua zinagombea kwenye nafasi hiyo ya kuandaa
michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017. Gabon imechaguliwa
dhidi ya Algeria na ghana. Libya ndio ingeliandaa michuano hiyo lakini
iliomba iondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na kudorora kwa usalama na
hali ya kisiasa ambayo imeendelea kusuasua.(P.T)
Gabon
itapokea michuano hiyo kwa mara ya pili, baada ya kushirikiana na nchi
nyingine kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2012.
Shirikisho
la soka barani Afrika CAF limeichagua Gabon dhidi ya Ghana, ambayo
imeshapokea michuano hiyo mara nne, pamoja na Algeria ambayo huenda
imepoteza nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama katika viwanja vyake,
baada ya kifo cha mchezaji wa Cameroon, Albert Ebossé, Agosti 23 mwaka
2014.
Libya
ambayo ingelipokea michuano hiyo, ilikua ilichaguliwa kupokea michuano
ya Kombe la mataifa ya Afrika katika mwaka 2013, lakini kutokana na vita
viliyokua vikirindima wakati huo, iliomba ibadilishwe katika maandalizi
ya michuano hiyo na iweze kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya
Afrika mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment