Ulaya kumaliza vifo vya Wahamiaji?
Picha za Kamera zikionyesha picha za baharini wakati wa Operesheni ya kuwaokoa wahamiaji
Mkuu wa
sera za kigeni ndani ya Umoja wa Ulaya amesema kuwa uharaka unahitajika
katika kushughulikia majanga yanayojitokeza katika bahari ya
Mediterania.
Federica Mogherini ameainisha mambo tisa ya mpango wa kumaliza tatizo la vifo vya wahamiaji.
Operesheni ya uokoaji itaimarishwa na kutakuwa na Kampeni maalumu ya kuteketeza boti zilizotumiwa kusafirisha watu.
Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema Roma ina mpango wa kupambana na wale waliowaita Wafanyabiashara wa utumwa.
Imeelezwa kuwa hatua zitachukuliwa kupunguza idadi ya wahamiaji na kuwarejesha wale wanaoingia barani Ulaya.
Mpango huu utajadiliwa na Viongozi wa Ulaya siku ya Alhamisi.
Wakati hayo yakijiri,Polisi nchini Italia inawashikilia watu wawili miongoni mwa walionusurika kwenye ajali ya boti.
Mtu mmoja
mwenye asili ya Tunisia ambaye anaaminika kuwa nahodha wa chombo hicho
na mwenzake Raia wa Syria walikamatwa wakishukiwa kuhusika na vitendo
vya kusafirisha watu kinyume cha sheria.
Watu hao walikamatwa baada ya meli moja yenye manusura wa ajali kuwasili katika bandari ya Catania katika kisiwa cha Sicily.BBC
No comments:
Post a Comment