Huenda 800 waliangamia baharini
Mashua ya wahamiaji iliyozama.
Federica Mogherini
Umoja wa
Mataifa unasema unahofia kuwa huenda watu 800 walifariki siku ya
Jumapili, pale mashua waliyokuwa wakilitumia kuvuka bahari ya
Mediterenean ilipozama karibu na Libya.
Shirika
la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limekuwa
likizungumza na manusura baada ya kuwasili katika kisiwa cha Sicily
mapema leo Jumanne.
Federica
MogheriniMkuu wa sera kwenye Muungano wa Ulaya Federica Mogherini
anasema kuwa pana haja ya kuwepo hatua za haraka ili kushughulikia suala
kuhusu wahamiaji katika bahari ya Mediterranean, huku akizindua
mikakati kumi ya mpango wa kutanzua vifo vya wahamiaji.
Mogherini,
anasema kuwa mipango hiyo ni hatua kubwa ya kuzuia kupotea kwa maisha
ya watu. Majukumu ya muungano huo ni kuzidisha operesheni ya uokozi,
pamoja na mipango mipya ya kuharibu mashua zinazotumiwa na walanguzi wa
binadamu wanaowavusha watu baharini.CHANZO:BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment