Ethiopia yaanza siku 3 za maombolezi
Islamic
State wakienda kuwaua raia wa Ethiopia.
Ethiopia imeanza siku tatu za
maombolezi ya kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na wanamgambo
wa kundi la Islamic State nchini Libya.
Bendera
zitapepea nusu mlingoti wakati nalo bunge la nchi hiyo likikutana
kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi
ya ishirini.
Msemaji
wa serikali Redwan Hussein, alisema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa
wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.
Mungano
wa Afrika ambao una makao yake makuu nchini Ethiopia ulilaani mauaji
hayo na kusema kuwa utafanya mikakati ya kuhakikisha kuwepo usalama
nchini Libya.
Wanamgambo
wa Islamic State walitoa kanda ya video ambayo inakisiwa kuonyesha
mauaji hayo yanayoonyesha watu hao wakipigwa risasi na kukatwa vichwa.CHANZO:BBC(V.S)
No comments:
Post a Comment