Machafuko Burundi, bajeti ya TZ 2015/2016 .. Uzinduzi wa Meli za Kivita TZ..
Nimekusogezea hizi story mtu wangu ni zile zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo April 29, Power Breakfast @CloudsFM ikafanya uchambuzi..
Wananchi wa Burundi wameonekana wakiwa
wamekusanyika katika mpaka wa Tanzania kutokana na machafuko
yanayoendelea kwao, Waziri wa fedha Saada Mkuya leo atawasilisha mwelekeo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Mbunge James Mbatia ameitaka Serikali kutoa tamko kutokana na kuporomoka kwa shilingi.
Nyingine iliyosikika ni Rais Kikwete kuzindua meli mbili za kivita zitakazotumika kufanya doria Baharini, Rais mstaafu wa Marekani Bill Clinton amewasili nchini kwa mazungumzo na Rais Kikwete, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ametunukiwa
Tuzo ya kutambua harakati zake za kutetea haki za binadamu na kuna
stori yya Jeshi la Polisi kulaumiwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha
kuliko wenye kipato cha chini.
Kulikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Shaaban Mwinjaka
ambae amezungumzia makubaliano waliyoyafanya baada ya kukutana na
SUMATRA pamoja na wamiliki wa mabasi kuhusu bei mpya ya nauli
iliyotangazwa.
No comments:
Post a Comment