Majimbo yapasua kichwa wana-Ukawa
Mwenyekiti wa Ukawa, Profesa Ibrahim Libumba.
HATIMA
ya kuachiana kwa majimbo ya uchaguzi kwa vyama vya siasa vya upinzani
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), inatarajiwa kujulikana
wiki ijayo.
Itajulikana
baada ya mkutano baina vyama washirika, uliolenga kutaka kufikiwa kwa
mwafaka wa ugawanaji wa majimbo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka
huu.
Hayo
yamethibitishwa na mmoja wa viongozi wa Ukawa, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Vyama
vingine vinavyounda umoja huo ni Chadema inayoongozwa na Freeman Mbowe,
NCCRMageuzi ya James Mbatia na NLD ya Dk Emmanuel Makaidi.
Alikuwa
akizungumza na gazeti hili juzi mjini hapa juu ya mchakato wa
makubaliano ya majimbo, ambayo baadhi yamezua mvutano ndani ya Ukawa.
Kwa Lipumba, suala hilo limepangwa kumalizwa Aprili 28, mwaka huu jijini
Dar es Salaam, ambapo viongozi vinavyounda umoja huo vitatu watakutana.
Aliwataja
viongozi kutoka vyama hivyo, watakaohusika katika majadiliano ya kina
ni pamoja na wenyeviti wa vyama, makamu wenyeviti, makatibu na wajumbe
wa sekretarieti kutoka ndani ya vyama hivyo watakuja kufikia makubaliano
ya mwisho.
Ukawa
ulianzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu la Katiba baada
ya kushikamana katika kulipinga bunge hilo la kihistoria na baadaye
kususa, kabla ya kusaini makubaliano kwa ajili ya kusimamisha mgombea
mmoja katika nafasi zote kuanzia udiwani, ubunge na urais.
Hata
hivyo, Lipumba alisema baada ya majadiliano ya muda mrefu ya viongozi wa
Ukawa kuhusu Umoja wao, kulijitokeza mvutano wa kuachiana majimbo
kadhaa, ambapo kila chama kilidai kinakubalika kwenye maeneo hayo na
hivyo suala hilo kuachwa kulifanyiwa kazi kwa kina zaidi.
"Majimbo
yote bado kufikiwa mwafaka wa pamoja na sasa tumepanga kukutana Aprili
28, mwaka huu Dar es Salaam kuweza kuweka wazi juu ya majimbo haya,"
alisema Profesa Lipumba.
Alisema
kwa Jimbo la Morogoro Mjini pia bado maafikiano yanaendelea na kwamba
moja ya sifa ni kuweka mgombea anayekubalika na wananchi wote.
Katika
taarifa yake kwa umma hivi karibuni, Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano,Tumaini Makene alisema Chadema na washirika wenzake wa
UKAWA, bado wanaendelea na mazungumzo ya kusimamisha mgombea mmoja kwa
nafasi za udiwani, uwakilishi, ubunge na urais katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, mazungumzo bado yanaendelea vizuri, hayajafikia
tamati na yakikamilika na makubaliano kufikiwa, viongozi wakuu wa UKAWA
watatoa taarifa rasmi kwa umma wa Watanzania. CHANZO: HABARI LEO (Muro)
No comments:
Post a Comment