Shambulio la kigaidi Nigeria, hili limehusisha kituo cha Redio
Nigeria ni moja ya nchi ambazo
zimeripotiwa kuwa na mashambulizi mengi yanayohusiana na ugaidi.. bado
kuna ripoti za mashambulizi mara kwa mara, bado pia kuna ishu ya
wasichana 270 abao walikamatwa na kundi la Boko Haram, mwaka mmoja umepita na bado hakuna dalili za wasichana hao kupatikana.
Leo kuna hii inayohusu watu wanne ambao wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya kituo cha Redio cha TA’O FM kilichopo eneo la Okene Jimbo a Kogi kulipuliwa kwa bomu jana usiku.
Bado haijafahamika sababu za kulipuliwa
kwa kituo hicho na hakuna kikundi chochote cha kigaidi ambacho kimedai
kuhusika na shambulio hilo mpaka sasa huku Polisi wakiendelea na
uchunguzi.
Waliofariki kwenye tukio hilo ni jamaa wanne ambao walikuwa walinzi wa Kituo hicho.
No comments:
Post a Comment