Kiongozi wa DA kutogombea uchaguzi ujao
Helen Zille kiongozi wa chama cha Democratic Alliance cha nchini Afrika Kusini
Kiongozi
wa chama cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance,DA,
amesema hatagombea katika uchaguzi wa chama hicho mwezi ujao.
Helen Zille amesema ni wakati muafaka kwake kutogombea, akisema kuwa DA watanufaika na mchango wa vijana.
Atabaki kuwa waziri mkuu wa jimbo la Western Cape hadi mwaka 2019.
Bi Zille, mwandishi wa habari wa zamani na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi amekiongoza chama hicho tangu mwaka 2007.
"Uamuzi wa aina hii ulikuwa ni muda mrefu, lakini mwishoni umefanyika ghafla," amesema.
Bi Zille
alizaliwa mwaka 1951 kwa Wajerumani wahamiaji. Alikuwa mtetezi wa katiba
ya kiliberali ya Afrika Kusini, akiwa mpinzani wa chama kikubwa cha
ANC.
Zamani, alimpinga waziwazi Rais Jacob Zuma na aliongoza kampeni ya kutaka afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za rushwa.
Bwana Zuma alikana madai hayo, akisisitiza kuwa yeye ni mwaathirika wa "njama za kisiasa".
Chama cha
DA kinaungwa mkono zaidi katika jimbo la Western Cape, ambalo lina
wakazi wengi weupe na machotara, lakini Bi Zille amejaribu kupenya
katika majimbo ya uchaguzi ya waafrika weusi.CHANZO: BBC (Muro)
No comments:
Post a Comment