Kiongera kurejea uwanjani
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam-shaffihdauda.com
'Simba
ililazimika kuusitisha kwa muda mkataba wa Kiongera baada ya Mkenya huyo
kutonesha majerahab yake ya muda mrefu ya goti na kulazimika kupelekwa
India kufanyiwa upasuaji.'
Kiungo
mshambuliaji wa KCB, Paul Mungai Kiongera, yuko mbioni kurejea uwanjani
baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na upasuaji wa goti
aliofanyiwa mwishoni mwa mwaka 2014.
Kiongera
ambaye yuko kwa mkopo KCB akitokea Simba SC ya Tanzania, bado hayuko
fiti kuichezea timu hiyo ya benki msimu huu kwa kuwa bado anaendelea
kutibu goti lake lililopasuliwa India mwaka jana.(P.T)
Kocha wa
KCB, Elvis Ayany, ameweka wazi alipohojiwa na mtandao wa futaa.comwa
Kenya leo kwamba mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Kenya kwa sasa
anafanya mazoezi mepesi na timu na huenda akarejea uwanjani katika muda
wiki chache zijazo.
"Kwa sasa
yuko fiti kimazoezi, amekuwa akifanya mazoezi na wachezaji wengine wa
kikosi chetu, ninaamini katika wiki chache zijazo anaweza kurejea
uwanjani, ni mcheza mzuri na sote tunajua ubora wake, kurejea kwake
kutakuwa msaada mkubwa kwa timu ukizingatia tunaelekea kumalizika
mzunguko wa kwanza wa ligi," amesema.
Timu hiyo ya benki imeyumba msimu huu wa Ligi Kuu ya Kenya; imeshinda mechi moja tu katika mechi nane za KPL.
No comments:
Post a Comment