SHEREHE YA UKUZAJI WA KISWAHILI YAENDELEA WASHINGTON, DC
Rais wa
CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu
Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha
Howard Washington, DC siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof
Venessa White Jackson.
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa
mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti
Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania
nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula .
Prof
Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae
kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria
sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015
katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
Ms
Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na
yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU
iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson '
Rais
mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa
kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili
hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.
Kutoka
kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi
wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Wanafunzi
wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa
kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.
Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU.(Muro)
No comments:
Post a Comment