NAPE AMSHUKIA DR. WILBOARD SLAA
KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye
KATIBU wa
NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,amekanusha taarifa zilizopo kuwa
chama hicho kinakisaidia Chama cha ACT Wazalendo akidai kuwa hawana
sababu ya kufanya hivyo.
Taarifa
kwa vyombo vya habari kutoka kwa Nape zinasisitiza kuwa CCM hakina
sababu ya kusaidia chama kingine cha siasa hivyo uvumi huo ni uchafuzi
wa kisiasa.
Akizungumzia
kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema, Dk
Wilbroad Slaa,kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza kuandikisha
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ngome ya CCM alisema huo ni
upotoshaji uliokubuhu kwani tanzania nzima ni ngome ya chama hicho.
Alisema
ratiba ya NEC haijapangwa kimkakati kama alivyodai Dk Slaa na kila
mtanzania ataandikishwa kwa mujibu wa sheria hivyo kauli za kuwapotosha
na kuwapa hofu wananchi hazina mashiko.
"Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape.
"Kauli hizi za Dk Slaa mzee kama yule ni uthibitisho tosha kwamba wenzetu vyama vya upinzani hasa chadema siasa zao zina lengo la kuwagawa watu kikanda,kanda wanayoiona ni kaskazini, uthibitisho wa mbegu mbaya ya chuki," alisema Nape.
Alisema CC
M
wanalaani vikali siasa za namna hiyo kwani hizo sio hoja za msingi ila
ni za kuwagawa wananchi na kupandikiza chuki zisizokuwa na maana na
suala hilo linaonyesha jinsi wapinzani wanavyofanya siasa za kikanda.
"Tunayo
taarifa kwamba Dk Slaa,Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe pamoja na
Mwenyekiti wa Nccr-Mageuzi,James Mbatia walikaa vikao wakawatenga wenzao
wanaunda Umoja wa Katiba Mpya (Ukawa, ambao ni Mwenyekiti wa
CUF,Profesa Ibrahim Lipumba ambaye anatokea Tabora na DK Emmanuel
Makaidi ambaye anatoka Kusini, hao wote tunajua wanatoka mikoa
gani,"alisema Nape
Nape
alisema siasa za namna hii zinazigawa nchi na kinachoonekana ni kwamba
wapinzani wanajua kuwa watashindwa na ccm ndio maana wanatafta
sababu,hivyo anawatoa hofu wananchi kuwa kila mtu mwenye sifaa
ataandikishwa.
"Chadema
wanajua watawaangusha vibaya, hatuna mpango wa kutumia mizengwe
watanzania watatuchagua, waache kuwagawa watanzania kwa kutaka madaraka,
wanatakiwa kuwashawishi wananchi kujiandikisha kama CCM
tunavyofanya"alisema Nape
"Wanapandikiza
mbegu mbaya na chuki yenye lengo la kugawa watanzania,nchi hii ni moja
ina makabila 136 na tunaishi vizuri hizi siasa chafu hazifai,, maneno ya
hovyo ambayo hayastahili kusemwa na mtu mzima kama yule, watashindwa
ndio maana wanasema watu wanaandikishwa kiujanja ujanja, wameanza
kujenga mbinu za ajabu, wananchi wanatupenda na watazidi
kutuchagua,"alisema Nape
Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.(Muro)
Alivitaka vyama vya siasa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na waliache zoezi hilo liende kama lilivyopangwalilivyopangwa, wasiwajengee watu hofu, hii sio sawa.(Muro)
No comments:
Post a Comment