Mikakati kupambana na wahamiaji haramu
Viongozi
wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuongeza zaidi fungu la fedha katika
operesheni kudhibiti wahamiaji haramu, barani Ulaya.
Fedha
hizo zitasaidia kusaka na kuokoa wahamiaji haramu katika bahari ya
Mediterranean katika kudhibiti wimbi la wahamiaji hao wanaotaka kuingia
Ulaya kutokea Afrika kaskazini.
Baada ya
mazungumzo ya dharura mjini Brussels Ubelgiji viongozi hao pia
wameidhinisha njia za kukamata na kuteketeza meli zinazoonekana kutumika
katika biashara hiyo ya binadamu.
Nchi kadhaa za Ulaya zimeahidi kutoa meli, helikopta na nguvu kazi nyingine.
Kwa upande wake Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk amesema ushirikiano mzuri unahitajika na nchi wahamiaji hao wanakotoka.BBC
No comments:
Post a Comment