TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, April 9, 2015

Kikwete ateua Balozi mpya wa Saudia 


RAIS Jakaya Kikwete amemteua Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, uteuzi huo ulianza Machi 27, mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Mgaza alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la Pili na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Abdillah Omar, ambaye mkataba wake wa utumishi umekwisha.(V.S)

No comments:

Post a Comment