Vigogo 3 wasitishwa kazi Rubada
KAIMU
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA),
Aloyce Masanja na wenzake wawili wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za
ubadhirifu wa fedha na kujilimbikizia madaraka.
Viongozi
wengine waliosimamishwa kuanzia jana ni Mkurugenzi wa Mipango na
Uwekezaji, Tatu Ndatulu na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Filozi
Mayayi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika,
Stephen Wassira alisema baada ya kuwepo kwa malalamiko yaliyokuwa
yanatolewa na wawekezaji kwa muda mrefu, serikali iliamua kuunda Tume
Novemba mwaka jana.
Tume hiyo
ilikuwa chini ya Semroki Mwanyika, ambaye sasa ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Ukaguzi wa Ndani wa Serikali katika Wizara ya Fedha (Hazina).
Wassira
alifafanua kuwa viongozi hao wanasimamisha kazi kwa tuhuma za kuiibia
Serikali kwa miaka miwili, utovu wa nidhamu na kushindwa kutimiza
majukumu yao kikamilifu kama watumishi wa umma.
Pia
alisema licha ya kuwasimamisha kazi viongozi hao, ripoti iliyoibua
ubadhirifu huo, itapelekwa katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) na Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili hatua za
kisheria zichukuliwe.
“Mimi
kama Waziri nimeamua kuwasimamisha kazi watu hao kutokana na
kutowajibika ipasavyo katika nyadhifa zao, pia wamekuwa watovu wa
nidhamu. Suala la makosa ya jinai nitawaachia Polisi na Takukuru ambao
watajua ni lini watawafikisha katika vyombo vya sheria,’’ alisema
Wassira.
Waziri
huyo alieleza katika miaka hiyo miwili, Rubada walikusanya zaidi ya Sh
bilioni 2.7 kutoka kwa wawekezaji. Aidha, alisema kati ya hizo, Sh
milioni 740 tu ndizo zilizotumika kihalali, huku kiasi kingine kikiwa
hakijulikani kilipo.(V.S)
Alifafanua
kuwa, kati ya zilizotumika, Sh milioni 13.9 imeelezwa zimetumika kwa
matumizi yao binafsi huku Sh milioni 13 zimetumika kwa ajili ya masurufu
ambayo hayajarudishwa.
‘’Pamoja
na hayo, Sh milioni 326 zilitengwa kwa ajili ya kujenga Kambi ya Kilimo
maeneo ya Mkongo na hazikufanya kazi iliyotakiwa. Pia walichukua Sh
milioni 58 ambazo zilitakiwa zipelekwe Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), lakini hazikupelekwa,’’ alidai.
Aliongeza;
‘’Kwa maana hiyo wafanyakazi walioko kazini kwa sasa wakistaafu,
hawataweza kulipwa mafao yao kutokana na pesa zilizotakiwa kupelekwa
hazijafikishwa sehemu husika’’.
Hii ina
maana kwamba, mbali ya Sh bilioni 2 ambazo hazijulikani zilipo, kiasi
kingine cha Sh milioni 384 kutoka mradi wa kambi ya Kilimo Mkongo na
zile za NSSF, jumla ya fedha ambazo hazijulikani zilipo ni Sh bilioni
2.3.
Wassira,
mmoja wa wanasiasa na viongozi wakongwe walioshika nyadhifa za uwaziri
tangu enzi za utawala wa Awamu ya Kwanza chini ya Rais Julius Nyerere,
alidai watumishi hao walikuwa wanatembea na fedha mifukoni, wakijifanya
wao ni wahasibu, ambapo fedha nyingine walikuwa wanaweka kwenye akaunti
ya serikali huku nyingine wakiweka katika akaunti zao binafsi.
Aidha, alisema Rubada kulikuwa na uongozi mbaya kwa kuwa na ubinafsi, rushwa na kwamba mfumo wa ndani ulikuwa na ubadhirifu.
Akizungumzia
suala la uteuzi wa viongozi wapya, Wassira alisema ameiagiza Bodi ya
mamlaka hiyo kutafuta watu weledi na waaminifu, watakaokaimu nafasi
hizo.
Akijibu
swali kuhusu ubadhirifu unaofanywa na viongozi wanaokaimu nafasi
mbalimbali, alisema; ‘’Suala la kukaimu sio sababu ya kuwa fisadi na
kuwa mbadhilifu wa fedha za serikali, kwani wapo wengine wanakaimu na
wanafanya vizuri hata kuthibitishwa na kuwa wakurugenzi.’’CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment