Semina ya Texas Karate Black Belts yafanyika Houston, Texas
Texas
Black Belts club Seminar , imeandaliwa na Sensei Ramon Veras, Dan 7,
Okinawa Goju Ryu Kyokai, mjini Houston, Texas tarehe 19 April, 2015. Pia
ni sehemu moja ya maandalizi na marekebisho ya mbinu na ufundi wa
vipande tofauti katika mfumo mzima wa Sanaa na tayari kwa baadhi ya
washiriki kwa msafara wa kwenda kwenye chimbuko la Karate huko Okinawa,
Japan.
Sensei Rumadha Fundi, ni mmoja ya wawakilishi wa Goju Ryu Jundokan, atayoiwakilisha Tanzania kwenye msafara huo..
Baada ya
takriban miaka 23 sasa, sensei Rumadha Fundi "Romi", anarejea tena chini
Japan kama alivyofanya mwezi May mwaka 1992. Safari hiyo ya mwezi June
kwenda Naha City, Okinawa kwa njia ya Los Angeles, Tokyo na hatimaye
Naha City, Okinawa.
Sensei
Rumadha amepewa mwaliko kama mwakilishi wa Jundokan Tanzania, kwa niaba
ya kuwa mteule na mwakilishi wa chama hicho cha mtindo wa Okinawa Goju
Ryu, chini ya rais wake ambaye ni mtoto wa Eiichi Miyazato mwanzilishi
wa chama hicho Sensei Yoshihiro Miyazato "Kancho", na hatimae kupewa
jukumu la kusambaza Jundokan nchini kote akiwa"Tanzania Chief Instructor
" na kupewa madaraka ya kutowa idhini na mikanda ya wawakilishi wa
Jundokan nchini Tanzania na utambulisho wa kutowa vyeti ( Dan
Certificate) kutoka, Naha, Okinawa.
Sensei
Rumadha anashikilia Dan 6 toka Tanzania Karate-do Federation, na Dan 3
toka Jundokan Kyokai.Lengo na madhumuni ya sensei Rumadha ni kusambaza
ufanisi wa Goju Ryu na mbinu za "Muchimi" ni undani halisi wa utumiaji
mbinu kifasaha na kitamaduni kama ifanyavyo huko Okinawa, Japan.
Sensei
Rumadha, atafanya mazoezi katika dojo ambayo mwalimu wake yeye Sensei
Bomani na Master Morio Higaonna walikuwa wanafunzi hapo miaka 45-50
iliyopita. Pia Sensei Rumadha, atatembelea sehemu zenye historia ya
mwanzao wa Karate na makaburi ya waanzilishi wa Sanaa na makumbusho ya
Karate na vitongoji vyake kama, Naha, Shuri na Tomari, Okinawa , Japan.
Nia na
madhumuni makubwa ni kutaka kuiendeleza Goju Ryu Karate Tanzania na
hatimae kuwa na walimu wenye utambulisho huko, Okinawa, Japan na kuleta
maendeleo na maslahi ya kimaisha kama mwalimu wa Karate.
Pia
Sensei Rumadha alisema " Tapenda kubadilisha mfumo wa jinsi Goju Ryu
inafundishwa Tanzania. Tawapa mwaliko wanafunzi wote wenye nia ya
mafanikio na utambulisho toka Okinawa, kuwa chini ya uongozi wangu na
kuendeleza utamaduni wa Goju Ryu. Goju Ryu ina matawi mengi na uongozi
tofauti, mimi napendelea kuwa na shina la Okinawa Goju Ryu Karate – do,
lililowekwa na waanzilishi wa mtindo huo; lengo ni kuwa na Goju Ryu
halisi na sio mabadiliko", alisema Sensei Rumaha.(Muro)
No comments:
Post a Comment