Hayajasahaulika ya New York, Ferguson.. Marekani bado kuna headlines za machafuko kutokana na ishu ya Ubaguzi.
Machafuko mengine Marekani, waandamanaji
wameingia mtaani.. wamepora vitu madukani, majengo yamechomwa moto..
bado kisa hiki kinahusishwa na ishu ya ubaguzi wa rangi kwa upande
mwingine.
Kijana Freddie Gray alifariki akiwa mikononi mwa Polisi, vurugu zikaanza muda mfupi baada ya kufanyika mazishi yake.
Kifo cha Gray
ambaye ni Mmarekani mweusi alifariki siku chache baada ya kulazwa
Hospitali akipatiwa matibabu ya majeraha aliyopata kwenye uti wa mgongo
baada ya baada ya kupigwa na Polisi.
Watu waliingia mtaani kufanya maandamano
ya kupinga kitendo kilichofanywa na Polisi, baadae hali ikabadilika,
majengo yakaanza kuchomwa moto na watu wengine wakaanza kuvamia maduka
na kufanya uporaji.
Waandamanaji hao walikuwa wakirusha mawe
kuyashambulia magari ya Polisi, majengo pamoja na kufanya uharibifu
mwingine huku maofisa wa Polisi 15 kujeruhiwa.
Watu 27 wamekamatwa kwa kuhusika na
matukio ya uporaji katika maduka ya pombe, dawa na maduka ya
kubadilishia fedha pamoja na kuwashambulia maafisa wa Polisi.
Kifo cha Gray
kilitokea April 19, hii iishu ni moja ya ambazo zimewahi kusikika
zikihusishwa na suala la Polisi wa Marekani kuwaua Wamarekani weusi..
iliwahi kutokea pia Jiji la Ferguson na New York.
Kwa sasa shughuli nyingi Baltimore
zimesimama, shule zimefungwa huku vikosi vya zimamoto vikiendelea na
jitihada kuzima moto pamoja na Polisi kuwatawanya waandamanaji.
No comments:
Post a Comment