TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, July 30, 2015

MANULA AIPELEKA AZAM FC NUSUFAINALI KAGAME CUP

Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza golipa wao Aishi Manula baada ya kudaka penati iliyopigwa na Hajji Mwinyi na kuivusha timu yake hadi kwenye hatiua ya nusu fainali ya Kagame
Wachezaji wa Azam FC wakimpongeza golipa wao Aishi Manula baada ya kudaka penati iliyopigwa na Hajji Mwinyi na kuivusha timu yake hadi kwenye hatiua ya nusu fainali ya Kagame
Timu Azam FC ‘Wanalambalamba’ wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuitupa nje ya mashindano timu ya Yanga kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Timu hizo zililazimika kufika hadi kwenye hatua ya mikwaju ya penati kufuatia kumalizika kwa mchezo huku timu hizo zikiwa sare ya bila kufungana. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya Kagame, hatua ya robo fainali inapomalizika ndani ya dakika 90 bila timu kufungana zinakwenda moja kwa moja kwenye changamoto ya mikwaju ya penati.
Aishi Manula alipangua penati ya Haji Mwinyi ambayo ilikuwa ni penati ya tatu kwa upande wa Yanga na kufanikiwa kuivusha timu yake hadi kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo penati za Azam zote ziliwekwa kambani.(P.T)
Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao, Pascal Wawa na Agrey Morris walifunga mikwaju yao kwa upande wa Azam wakati Salum Telela, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Godfrey Mwashiuya walifunga penati zao huku Hajji Mwinyi yeye penati yake ikidakwa na mlinda mlango wa Azam FC Aishi Manula.
Mpira ulianza kwa kasi sana dakika za mwazo za kipindi cha kwanza, huku Azam wakifanya shambulizi kali dakika hiyohiyo ya kwanza ambapo Kipre Tchethe alishindwa kufunga goli baada ya Shah Farid Mussa kupiga krosi iliyowapita walinzi wa Yanga na kumkuta yeye ambae aliukosa mpira.
Azam hawakuishia hapo waliendelea kufanya mashambulizi lakini wachezaji wa Azam hawakuwa makini kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa wamekosa takribani nafasi nne za kufunga.
Kwa upande wa Yanga, kipindi cha kwanza hakikuwa kizuri sana kwao kwasababu hawakufanya mashambulizi mengi ambayo yaliwashtua Azam. Shambulizi lililofanywa na Yanga lilitokana na mpira wa kurusha ambapo Mbuyu Twite alirusha mpira uliookolewa kwenye mwamba wa pembeni wa goli na mlinda mlango Aishi Manula.
Wachezaji wa Azam walikuwa wakitumia nguvu nyingi sana kuwakaba wachezaji wa Yanga hali ilyopelekea mwamuzi kuwatuliza kwa kuwapa kadi za njano. Kheri Abdullah Salum, Frank Domayo, Jean Mugiraneza na Ame Ally walioneshwa kadi za njano baada ya kuwachezea vibaya wachezaji wa Yanga. Wakati kwa upande wa Yanga Juma Abdul na Mbuyu Twite walioneshwa kadi za njano.
Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kreri Abdullah Salum na nafasi yake ikachukuiwa na Said Morad wakati Frank Domayo ‘Chumvi’ alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ally ‘Zungu’. Yanga wao wakamuingiza Salum Telela kuchukua nafasi ya Deus Kaseke wakati Juma Abdul alitoka kumpisha Joseph Zutah na Malimi Busungu akaingia baada ya Amis Tambwe kupumzishwa.
Kipindi cha pili bado Azam waliendelea kukosa magoli kwani Kipre Tchetche, Ame Ally na Shah Farid Mussa walikosa goli baada ya kujichanganya wao kwa wao na mpira kunyakwa na mlinda mlango Ally Mustafa ‘Barthez’
Kwa matokeo hayo, Azam FC inakamilisha timu nne zilizofuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame kwa mwaka 2015 ambapo Ijumaa itakutana na KCCA ya Uganda iliyofuzu kucheza hatua ya nusu fainali leo mchana kwa kuibanjua timu ya Al Shandy ya Sudan kwa goli 3-0 huku Yanga wakiwa wameyapa mkono wa kwaheri mashindano ya Kagame kwa mwaka 2015.
Chanzo:Shaffihdauda.com

Maoni ya viongozi wa Afrika kuhusu hotuba ya Obama 

" Hakuna mtu anapaswa kuwa rais wa milele ", amesema Rais Obama katika hotuba yake kwa Umoja wa Afrika, akiwakemea viongozi wa Afrika wenye nia ya kusalia madarakani wakati muda wao wa kuondoka madarakani unapofika mwisho.
Na RFI
Rais wa Marekani Barrack Obama ametamatisha ziara yake barani Afrika, kwa ujumbe kwa viongozi wa bara hilo kuondoka madarakani muda wao unapofika mwisho.
Akizungumza katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addis Ababa Jumanne wiki hii, Obama amewaambia viongozi wa Afrika kuwa tabia ya kukataa kuondoka madarakani inarudisha nyuma maendeleo ya demokrasia.
Ujumbe wa Obama ulimlenga rais wa Burundi Piere Nkurunziza ambaye alikataa kuondoka madarakani pamoja na viongozi wengine wanaobadilisha katiba ili kuendelea kusalia madarakani.(P.T)
Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ametupilia mbali kauli za viongozi wa nchi za kigeni.
" Rais Obama amerejelea maneno tunayosikia tangu miezi kadhaa kutoka kwa viongozi kadhaa wa Magharibi ambao, wakati wanatembelea Afrika, hawawezi kujizuia kutoa mafunzo kwa nchi za Afrika kama vile Afrika imekua nchi moja, ikiwa na tatizo moja na ufumbuzi mmoja, kana kwamba Afrika imekua na utaratibu wa Marekani kuhusu muda wa marais madarakani. Lakini sisi katika DRC tunahisi kuwa jambo hilo halituhusu, ingawa tunaona kuwa ni muhimu kuja na kutuambia jinsi ya kutatua matatizo yetu ya kitaasisi ... ", amesema Lambert Membe.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, amekaribisha hotuba ya rais Barack Obama juu ya haja ya kuimarisha demokrasia barani Afrika. Waziri Mkuu wa Ethiopia, hata hivyo, alionekana akikosolewa na Barack Obama kwa kuwanyanyasa na kuwazuia jela waandishi wa habari pamoja na kuwa kandamiza wapinzani.

Akon kuleta umeme Afrika 

Muimbaji wa miondoko ya R&b anayeongoza katika chati za juu za muziki huo duniani 'Akon' ameamua kutumia tasnia yake ya muziki kukabiliana na maendeleo endelevu ya watu wa barani Afrika.
Nyota huyo wa R & B anazindua mpango maalumu wa mafunzo unaoitwa "Akon Angaza Afrika" ambao una lengo la kutumia nguvu ya jua kuzalisha umeme huku akiwa na matumaini ya kuwafikia watu milioni 600 barani wa Afrika.
Ufunguzi wa huo umefanyika mjini mkuu wa Bamako nchini Mali, baadaye mafunzo hayo yatafundisha kwa wadau wa mradi huo jinsi ya kutunza mifumo ya nishati hiyo inayoendeshwa kwa nguvu ya jua.
Samba Bathily ambaye ni mwanzilishi msaidizi wa mradi huo, anasema jua na teknolojia hiyo ya ubunifu itasaidia kuleta umeme katika nyumba na kwenye jamii kwa ujumla.
Kwa sasa anasema kuwa wanaimarisha utaalamu wa Kiafrika na kwamba hilo ni lengo lao.
Ameelezea sababu ya kuwekeza zaidi kwenye nishatiya umeme kwamba ni moja ya njia ya kutoa fursa za kiuchumi na huduma za kijamii kwa bara la Afrika ambalo sehemu kubwa ni giza kutokana na ukosefu wa Nishati.

Maelezo yaliyotolewa na Polisi Dodoma kuhusu Naibu spika Job Ndugai kumpiga mtu mpaka akazimia.

Ndugai 1 
Stori ilianza kusambaa kuanzia July 28 2015 kwamba Naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai amempiga mtu mpaka akazimia na kisha baadae kufariki.
Hili tukio limefanya mpaka millardayo.com imtafute kamanda wa Polisi Dodoma Kamishna msaidizi mwandamiz wa Polisi David Misime ambaye ameyathibitisha haya >>> ‘Ukweli nilionao mimi ni kwamba tarehe 28 2015 jioni Joseph Elieza Chilongale alifika kwenye kituo cha Polisi Kongwa Dodoma akilalamika kuwa wakiwa kwenye mkutano wa kujinadi kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kongwa kupitia CCM, alipigwa kwa kutumia fimbo kichwani na tumboni na Job Ndugai
Baada ya kutoa taarifa hiyo alipewa PF3 na akapelekwa Hospitali ambako amelazwa, tunachofanya ni kuendelea na uchunguzi kwa kupata maelezo kutoka kwenye eneo la tukio kutoka kwa watu waliokuwepo pale na baada ya kukamilisha upelelezi tutafikisha jalada kwa Mwanasheria wa serikali aelekeze hatua za kuchukua‘ – Kamanda Misime.
Kuhusu taarifa kwamba Joseph amefariki, Kamanda Misime amesemahizo taarifa sio za kweli sababu mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kongwa muda mfupi uliopita alikua pale Hospitali kuchukua maelezo yake kwa ajili ya kukamilisha upelelezi

Picha na maelezo kuhusu hii Treni iliyopata ajali Dodoma July 29 2015

tr
Hii post ni maalum kwa ajili ya kuujua ukweli baada ya ajali ya Treni iliyotokea kwenye tarafa ya Kikombo Dodoma ambapo mabehewa manne ya Treni hii ya abiria kutoka bara kwenda Dar es salaam yaliacha njia.
Kamanda wa Polisi Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime amesema saa tatu na dakika 45 asubuhi, mabehewa manne yaliacha njia na kusababisha ajali lakini hakuna yeyote aliyejeruhiwa.
tr2
Amesema chanzo cha ajali hakijafahamika ila ajali imetokea wakati treni ikiwa kwenye mwendo katika stesheni ya Kikombo kuelekea kusimama, injini na Mabehewa hayo yakiwa kwenye mwendo yalihama njia ambapo July 29 2015 zilifanyika jitihada za kufaulisha abiria katika mabehewa mengine pamoja na kuunga injini nyingine ili safari iendelee.tr3

Sababu ya Mbwana Samatta kugoma kujiunga na Zamalek ya Misri

Samatta 
Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa kimataifa kutokea Tanzania anaeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo alijiunga nayo mwaka 2011 akitokea Simba ya Tanzania na mpaka sasa amekua mmoja kati ya wachezaji mahiri wanaounda safu imara ya ushambuliaji kwa TP Mazembe na timu ya taifa ya Tanzania.
samata 
Samatta aliingia kwenye headlines siku kadhaa zilizopita baada ya kukataa kusajiliwa na klabu ya Zamalek ya Misri kwa euro milioni 1 kutoka TP Mazembe ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 2.3 za Kitanzania, kila media iliandika hii story nakuonekana kama Samatta amepoteza bahati.
Wakala wa mchezaji huyo Jamal Kasongo amezungumzia suala hilo na mpango wa Samatta licha ya kupewa ofa ya mshahara mkubwa.
Mbwana-2 
“La kwanza ni kweli maafisa wa Zamalek wawili walifika kipindi mimi nipo na Mbwana kipindi yupo katika mechi ya timu ya taifa kimsingi mimi niliweza kukaa nao chini kuweza kufanya nao majadiliano lakini lazima mchezaji ili ufikie malengo uweze kukaa katika mstari, msimamo wa Mbwana na msimamo wangu mimi kama mshauri wake ni Mbwana kuweza kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
MbwanaSamata-inaction120712BBP300 
“Wakatuma tena ofa wako tayari kumnunua TP Mazembe kwa euro milioni 1 na euro milioni 1 ni pesa nyingi na walikuwa tayari wakimuhitaji waweze kumpa mshahara ambao hakuna mchezaji ndani ya Afrika hii anaweza akalipwa lakini bado hili suala lilikuwa gumu kwani lengo kubwa ni Mbwana kucheza Ulaya”>>>Jamal Kasongo
Mbwana Samatta anamaliza mkataba wake na TP Mazembe mwezi April 2016 hivyo anaweza kuwa mchezaji huru na kuchagua timu ipi ya kwenda

Tuesday, July 28, 2015

Hili ni jingine la kulijua kwenye familia za Cristiano Ronaldo na Messi.

lionel_messi_vs_cristiano_ronaldo 
Upinzani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kuhusu nani bora zaidi ya mwenzake huwa ni mgumu kutupatia majibu yaliosahihi kwa maoni ya watu hususani ukihusisha mashabiki wa pande zote mbili, hata zile tuzo zinazotolewa za mchezaji bora wa dunia (Ballon D’or) huwa hazitoshi kuwaridhisha mashabiki wa upande mmoja kuwa kwa mwaka huu flani ni bora zaidi ya mwenzie.
6057156223960338_20779271aa1c14ea9a0610f309660daf5c8c2c6a80e1f69f27ed706f81fe23ef_largeSasa wataalamu wa mambo wamejichunguzia na kugundua kwamba Ronaldo kazaliwa February 5 1985 na Lionel Messi amezaliwa June 24 1987 ikiwa ni tofauti ya miaka miwili na miezi kadhaa tofauti hiyo ukiibadili kwa siku Ronaldo kamzidi Messi siku 869.
tumblr_nbsq17lud31rm96xko3_250 
Messi ana mtoto anaitwa Thiago na wa Cristiano ni Cristiano Ronaldo Jr cha kushangaza hapa ni tofauti ya siku iliyopo kati ya Thiago na Ronaldo Jr, mtoto wa Ronaldo ni mkubwa kwa Thiago na amempita kwa siku 869, hii ni sawa kabisa na tofauti iliopo kati ya Messi na Ronaldo
87d47013aa807fe6f5b64d4fa951a5ae

Maneno ya James Mbatia alivyomkaribisha Edward Lowassa UKAWA

image 
Headlines baada ya headlines kuhusu siasa Tanzania zina uzito mpya kila siku… Imeandikwa sana Magazetini kuhusu Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa kuhama CCM, kilichoteka headlines July 27 2015 kimeongezea uzito kwenye ishu hiyo.
Viongozi wa Vyama vya UKAWA, Emmanuel Makaidi, Prof. Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wamekutana Makao Makuu ya CUF Buguruni Dar na kutoa majibu kuhusu kumpokea Edward Lowassa.
Uchaguzi wa October 2015 ni fursa ya kipekee ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu kuondoa ukandamizi uliojikita CCM… Watanzania wanahitaji Mabadiliko yenye fikra mpya na bunifu kwa maslahi ya Watanzania wote“>>> James Mbatia.
UKAWA tunahitaji Viongozi wenye sifa, uwezo na weledi katika kulinda, kuheshimu na kusimamia rasilimali za Taifa kwa maslahi ya Taifa.. Nachukua fursa hii kumualika Mheshimiwa Lowassa ajiunge na UKAWA na tuko tayari kushirikiana nae kuiondoa CCM madarakani” >>>> James Mbatia.
Bado Mbunge Edward Lowassa hajajibu chochote kuhusu kuendelea na CCM au kuhama

Hii ndio timu iliofanikiwa kunasa saini ya Drogba

accrareport_didier-drogba-retires-from-international-football
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye pia amewahi kuitumikia klabu ya Chelsea ya Uingereza kwa miaka kadhaa sasa ameamua kuendeleza maisha yake ya soka Canada na ataanza kuonekana katika Ligi Kuu ya Marekani MLS.
DidiFinale12
Taarifa zimethibitisha kuwa Drogba amekubaliana na klabu Montreal Impact  na atajiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi 18, Drogba amekuwa akiwindwa na timu zinazoshiriki Ligi Kuu Marekani toka mwaka 2012 na alikataa mshahara wa dola milioni 7.5 kwa mwaka na kutimkia China.
Didier Drogba celebrates Chelsea goal in FA Cup semi final win over Tottenham 2012
Rais wa klabu ya Montreal Impact Joey Saputo amethibitisha Drogba kujiunga na kikosi chao.
“Ni heshima kumkaribisha Drogba katika klabu ya Montreal Impact, toka mazungumzo yetu ya kwanza nazungumza nae, nilijisikia kwamba kiukweli alitaka kuichezea Montreal”>>>Joey Saputo 
CK8CB_rWgAAQBAz
Picha ya July 27 Drogba alipo kutana na Neymer Ibiza Airport
Drogba anaungana na mastaa wengine wa soka waliowahi kutamba katika Ligi Kuu Uingereza, mastaa hao ni Frank Lampard na Steven Gerrard bila kumsahau mkali mwingine kutokea Italia Andrea Pirlo amabo pia wametimkia Marekani.

CECAFA yatangaza mabadiliko haya na kutoa onyo kali kwa Gor Mahia na Kocha wake

IMG_5796
Baraka Kizuguto msemaji wa TFF
Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA limetangaza mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mechi za robo fainali ya michuano hiyo.. CECAFA imetangaza mabadiliko hayo kupitia kwa msemaji wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto.
cecafa
Mabadiliko yaliotangazwa hapo ni ya mechi za robo fainali, mchezo wa kwanza utapigwa saa 7:45 ambapo itakuwa mechi kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Khartoum ya Sudan na mchezo wa pili utapigwa saa 9:45 utakutanisha timu ya  Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini, michezo hiyo itapigwa July 28.
KMKM-vs-Gor-Mahia-1
Kikosi cha Gor Mahia ya Kenya
July 29 itapigwa michezo miwili wa kwanza utakuwa mchezo kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya AL Shandy ya Sudan saa 7:45 na mchezo wa pili ni kati Azam FC  dhidi ya Yanga saa 9:45 michezo yote itapigwa katika Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na hakutakuwa na dakika 30 za nyongeza kama timu zitatoka suluhu bali zitapigiana mikwaju ya penati.
NUTTALL-THINK
Kocha wa Gor Mahia Frank Nutall
Sambamba na mabadiliko hayo CECAFA pia imewaandikia barua ya kuwapa onyo klabu ya Gor Mahia ya Kenya na kocha wao Frank Nutall kwa utovu wa nidhamu kwa kutumia mlango ambao hawakupaswa kutumia wakati wa kuingia na kutoka vyumbani.

Jamaa aliachiwa mtoto mchanga akaamua kumnywesha maziwa aliyochanganya na pombe

bby grl
Dunia ina vituko vyake mtu wangu, na kwa wenzetu wa Marekani wakati mwengine vituko huzua madhara makubwa.
Nimekutana na hii moja inayomhusu Dontavian Eagle McCree mwenye miaka 19 aliyeachiwa jukumu la kukaa na mtoto wa dada yake wakati yeye akiwa kazini.
Dontavian-McCree
Siku moja wakati akiwa nyumbani na mtoto wa dada yake, Dontavian aliamua kumpatia mtoto huyo wa miezi 10 pombe, akachanganya pombe kwenye maziwa ya mtoto na kumnywesha.
Siku chache baadae mtoto alianza kuumwa na baada ya mama yake kugundua aliamua kumpeleka mtoto hospitali na ndipo alipogundua kuwa mtoto alinyweshwa pombe.
dddr
Dontavian Eagle McCree,19.
Dontavian amekamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na thamani ya dhamana yake ni dola 15,000 ambayo ni sawa na Mil.30 za Kitanzania. Hali ya mtoto sio nzuri kabisa.

Monday, July 27, 2015

Familia ya Bobby Brown yathibitisha kifo cha Bobbi Kristina

bobi kristina
Imepita miezi sita toka Bobbi Kristina mtoto wa marehemu Whitney Houston akutwe amepoteza fahamu bafuni kwake, na toka kipindi hicho amekuwa kwenye coma kwa muda mrefu hospitalini kabla ya familia yake kumhamishia nyumbani baada ya kuona hakuna matumaini ya ziada.
Familia ya Bobbi Kristina imeweka wazi kuwa mtoto pekee wa marehemu Whitney Houston amefariki 27 July 2015 baada ya kipindi kirefu cha kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Wanafamilia hao wana majonzi makubwa hasa wakiangalia kifo cha Bobbi ambavyo kimefanana kabisa na jinsi ambavyo mama yake mzazi, Whitney Houston alifariki.
Mipango ya mazishi yake inaendelea kufanywa, lakini kwa Nick Gordon huu ni wakati mgumu zaidi kwake kutokana na kushtakiwa kuwa mtu aliyehusika kutengeneza mazingira ya kifo cha Bobbi Kristina.
>>> “Sasa hivi tunataka kumzika binti yetu ili ampumzike kwa amani, lakini upelelezi mzito utaanza rasmi baada ya mazishi haya, yoyote yule aliyehusika kumsababishia mwanangu yote haya lazima mkono wa Sheria umpitie”. <<< Bobby Brown, baba wa Bobbi Kristina.

Saturday, July 25, 2015

Nkurunziza karudi madarakani Burundi? Haya ndio matokeo ya Uchaguzi..

NKURUZINZA
Uchaguzi Mkuu wa Rais Burundi umefanyika tayari japo kulikuwa na mvutano mkubwa sana kutokana na ishu ya kuonekana Rais Pierre Nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu ilikuwa ni kwenda kinyume na kanuni za nchi hiyo.
Matokeo yametolewa July 24 2015 na matokeo yameonesha Rais Nkurunziza ameshinda tena Uchaguzi huo kwa kupata 69.4% ya kura na kumshinda mpinzani wake wa karibu Agothon Ruwasa aliyepata 18.9 %. 
Kulikuwa na jumla ya Wagombea nane kwenye nafasi hiyo lakini Wagombea wengine walijitoa kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo.

Pichaz za Rais Obama wakati anatua Uwanja wa Ndege Nairobi Kenya…

IMG_2556
July 24 2015 Rais wa Marekani Barack Obama hatimae tayari ametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta muda mfupi uliopita, mapokezi yote yalioneshwa LIVE kwenye TV ya K24 ya Kenya.
Hapa nina pichaz kuanzia mwanzo kabisa alivyokuwa akishuka.
IMG_2551
IMG_2554
IMG_2560
IMG_2565
IMG_2568
IMG_2569
IMG_2575
IMG_2581
IMG_2589
IMG_2590
IMG_2598
IMG_2600
IMG_2617
IMG_2630
IMG_2638
IMG_2645
IMG_2651

Hatimaye Chris Brown karuhusiwa kuondoka Ufilipino… amesema haya kuhusu kuzuiliwa kwake!

BRR2
Baada ya kuzuiliwa kutoka nchini Ufilipino kwa siku mbili hatimaye Chris Brown kaachiwa huru na kuondoka salama kabisa… msanii huyo ambaye alikuwa mjini Manila kwa ajili ya show alizuiliwa kuondoka siku ya Jumatano kutokana na madai ya kuwa hakutimiza wajibu wake wa kimkataba kipindi cha Mwaka mpya kuingia 2015.
Chris Brown performs at the Black Entertainment Television awards show
Licha ya kuachiwa huru Chris Brown alichukua time na kupost Twitter kusema hakuhusika na madai hayo na alitimiza wajibu wake wa kimkataba kwani alirudi kutoa show nyingine kufidia show aliyoikosa mwaka mpya.
>>> “Manila mmetisha sana, nawapenda sana…ishu iliyotokea sio ndogo na aliyehusika kufanya hivi inabidi atafutwe, jina langu limetumika na sikufanya CHOCHOTE!!”<<< Chris Brown.
BRR3
>>> “Sihusiki na hizi tuhuma, nilirudi Manila kufidia show niliyoikosa mwaka mpya..”. <<< Chris Brown.
Chris Brown ana show nyingine jijini Macau usiku wa July 24 2015 na kwenye video aliyoipost Twitter amewahakikishia mashabiki kuwa atakuwepo Live kwa ajili ya kutoa show hiyo.