TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, April 29, 2014

Ukraine; Warusi zaidi wawekewa vikwazo 

140426122158_ukraine_512x288_ap_nocredit_6e081.jpg

Marekani imetoa taarifa kuhusu vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi na kuushutumu utawala wa Moscow kwa kushindwa kutimiza mkataba wa kimataifa uliolenga kusuluhisha mzozo wa Ukraine.
Vikwazo hivyo vimelenga washirika wa Karibu wa Rais wa Urusi Vladmir Putin na vimeongeza orodha ya vikwazo vilivyowekwa hapo awali kwa baadhi ya maafisa wa nchi hiyo baada ya Moscow kutwaa eneo la Crimea mwezi uliopita.
Miongoni mwa waliolengwa ni mmoja wa wanasiasa maarufu nchini Urusi Igor Sechinambaye wakati mmoja alikuwa afisa wa ujasusi na sasa ni afisa mkuu katika kampuni ya mafuta ya Rosneft ambayo kwa kiwango kikubwa inadhibitiwa na serikali.
Karibu asilimia sitini ya kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya mafuta ya uingeza BP na thamani ya hisa za kampuni hiyo ilishuka punde tu baada ya taarifa kuhusu vikwazo hivyo kutolewa.
Wengine waliolengwa ni Alexei Pushkov, ambaye huongoza kamati ya mambo ya nje katika bunge la Urusi,Naibu waziri mkuu na kampuni kumi na saba za Urusi.
Akizungumza hapo awali Rais Putin alisisitiza kuwa Ukraine haitaathirika kiuchumi kutokana na vikwazo hivyo.
Rais wa Marekani Barack Obama amesema nia ya Marekani sio kumlenga moja kwa Rais Putin lakini ni katika juhudi za kuishawishi Urusi kufuata mwelekeo unaofaa.
Muungano wa Ulaya pia umetangaza vikwazo vya usafiri na kuzuiliwa kwa mali dhidi ya watu 15 nchini Urusi lakini majina yao bado hayajatajwa.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment