HELIKOPTA YAANGUKA IKIWA IMEMBEBA MAKAMU WA RAISI
Taarifa
iliyoifikia kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya
jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka
uwanja wa ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na
kuangukia paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo
kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la
mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya
zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya
moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko
yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya
kulipuka.
Ndani ya Helikopta walikuwepo watu
mbalimbali akiwemo Makamu wa rais Dr. Bilal, Kamanda wa polisi kanda
maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Said Mecky Sadick.(Awadh Ibrahim)
No comments:
Post a Comment