TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, April 13, 2014

Hatari ya daraja Mbagala lililonyima magari kwenda mikoa ya kusini na ya kuingia Dar

62mbgl
Mvua zinazoendelea kunyesha mikoa tofauti Tanzania bado zimeendelea kuleta madhara ambapo pamoja na taarifa ya Watanzania kadhaa kukosa makazi na wengine kupoteza maisha bado barabara na madaraja vimezidi kubomoka.
Hizi picha ni za daraja la mto Mzinga ambalo ndilo linalounganisha Dar na mikoa ya kusini limeanza kumeguka kufuatia mvua iliyonyesha na inayoendelea kunyesha ambapo sasa Wasafiri wa kwenda Nachingwea, Masasi, Tunduru, Mtwara, Lindi na maeneo jirani wamekwama.
Baadhi ya kampuni ambazo zinamiliki zaidi ya mabasi manne, zimekua zikifaulisha wasafiri toka kwenye mabasi yaliyokwama upande wa Mtwara kuingia kwenye basi lililo upande wa Dar na wa Dar kuingia basi la Mtwara ili safari ziendelee.
Miongoni mwa wasafiri ambao wamekwama kusafiri ni pamoja na Tundaman ambaye alikua na show leo Maisha Club Mtwara.
4mbgl
Askari polisi wamekuwepo kwenye eneo la tukio ambapo wamekua wakivusha watu kwa mguu na kuwasindikiza, licha ya magari kutoruhusiwa kuvuka kwenye daraja hili, hata pikipiki zimepigwa marufuku kabisa.
63mbgl
64mbgl
49mbgl
52mbgl
50mbgl
47mbgl
43mbgl
42mbgl
45mbgl
35mbgl
26mbgl
Msanii wa bongofleva Tunda Man alikwamia Mbagala akiwa safarini kuelekea Mtwara.
27mbgl
29mbgl
22mbgl
21mbgl
19mbgl
13mbgl

No comments:

Post a Comment