Alichosema Samwel Sitta kuhusu maongezi yake na Rais JK pia viongozi wa dini
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema Rais Jakaya Kikwete anaonekana kuwa tayari kuongeza muda wa bunge hilo kuendelea kujadili vifungu vya rasimu ya pili ya katiba mpya baada ya bunge la bajeti kumalizika.
Muda
 uliotolewa toka mwanzo ni siku 70 yani ndizo zitatumiwa na bunge maalum
 la katiba kujadili vifungu 17 vya hiyo rasimu lakini siku hizo 70 ndio 
zinakatika Aprili 28 ambapo bunge hili la katiba mpaka sasa likiwa 
limejadili vifungu viwili tu vya rasimu ya pili ya katiba mpya. 
Namkariri
 Samwel Sitta akisema ‘nilionana na Rais Kikwete ili atafakari namna ya 
kuongeza muda wakati huohuo muelewe kwamba kule Dodoma inabidi tulipishe
 bunge na baraza la Wawakilishi ili bajeti ya nchi isisimame kwa sababu 
muda wake ni May na June’ 
Kuhusu maamuzi ya Samwel Sitta kukutana na viongozi wa dini askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama POLYCAP KARDINAL PENGO  na Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti ISSA BIN SHABANI SIMBA,
 amesema ‘nilitafakari nikaona ni muhimu tunapofikia hatua flani ya 
mchakato huu ni vizuri kwenda kwa viongozi wetu wakuu wa Madhehebu, 
lengo ni kuwapasha habari za nini kinachoendelea Dodoma, wajue tumetoka 
wapi, sasa hivi tuko wapi na matarajio yetu ni nini
No comments:
Post a Comment