Stori nyingine kubwa ya Egypt ni hii adhabu kwa Wapenzi wa jinsia moja
Stori
hii iliyoandikwa na BBC inasema >>> Mahakama moja nchini Misri
imewahukumu watu wanne kifungo cha hadi miaka nane jela kwa kosa la
vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja ambapo watu hao wanashutumiwa
kuhudhuria au kupanga tafrija za vitendo vya ngono, kuvaa mavazi ya
kike na kujipodoa.
Sheria
ya Misri haitamki kupiga marufuku vitendo vya mapenzi ya jinsia moja
lakini waendesha mashitaka wametumia sheria ya Misri inayokataza mambo
fulani kufanyika hadharani kuwahukumu wapenzi hawa wa jinsia moja.
Mmoja
wa watu hao amehukumiwa na mahakama ya Cairo kifungo cha miaka mitatu
jela na kazi ngumu huku kikundi cha kutetea haki za binadamu chenye
makao yake nchini Marekani, Human Rights First kikisema hukumu hizo
zinasikitisha na kukatisha tamaa.
Kikundi
hicho kimesema tangu kung’olewa madarakani Rais Mohammed Morsi mwezi
Julai 2013 kumekuwa na ongezeko la watu kukamatwa kwa misingi ya jinsia
zao.
Hukumu
ya sasa inakumbushia kesi ya mwaka 2001 ya watu 52 kushutumiwa kwa
vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na makosa mengine chini ya sheria ya
Misri ambapo 23 walihukumiwa kifungo cha kufikia miaka mitano jela
pamoja na kazi ngumu.
Kikundi
kimoja cha kutetea haki za binadamu nchini Misri kimesema adhabu kali
zilizotolewa kwa watu hao Jumatatu ni sehemu ya msako unaoendelea dhidi
ya uhuru binafsi.
No comments:
Post a Comment