TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, April 13, 2014

BREAKING: Mkuu wa mkoa kuhusu bomu lililolipuka Arusha April 13 usiku, idadi ya waliojeruhiwa.

Screen Shot 2014-04-13 at 11.35.19 PM
Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
millardayo.com imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana alietekeleza shambulio hilo.
Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.
Unataka niwe nakutumia stori kama hizi na kila nyingine inayonifikia? jiunge na familia ya millardayo.com kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo na nitafanya hivyo iwe usiku au mchana mtu wangu.

No comments:

Post a Comment