Kura aina ya Muungano Agosti
Upigaji
kura kupitisha sura mbili zinazohusu Muungano katika Bunge la Katiba
umesogezwa mbele hadi Agosti litakapoitishwa tena, Mwananchi limebaini.
Vyanzo
mbalimbali vimelidokeza gazeti hili jana kuwa upigaji kura hautafanyika
sasa badala yake wajumbe wa Bunge wataendelea kuchangia hoja hadi Aprili
28, mwaka huu wakati Bunge hilo litakapoahirishwa baada ya kukamilisha
siku 70 za awali.
Awali,
upigaji huo wa kura ambao umewagawa wajumbe katika makundi mawili; moja
likitaka serikali tatu na jingine likitaka serikali mbili, ulitarajiwa
kufanyika Ijumaa wiki hii ili kuhitimisha mvutano wa muda mrefu baina ya
pande zinazopingana.
Chanzo
chetu ndani ya Kamati ya Uongozi, kilidokeza jana kuwa hata baada ya
Bunge hilo kurejea Agosti 5, mwaka huu, ikielezwa kuwa lengo ni kutoa
fursa ya kuendelea kushawishi uungwaji mkono ili kupata theluthi mbili
ya kura inayohitajika.(MM)
Mwenyekiti
wa Bunge, Samuel Sitta alithibitisha kuahirishwa kwa upigaji wa kura
huo, lakini akasema hiyo imetokana na wingi wa wajumbe wanaotaka
kuchangia na si kitu kingine.
"Ni kweli
wajumbe hawatapiga kura kwa sura mbili walizowasilisha hadi jana na
lengo ni kuwapa nafasi wajumbe wengi zaidi kuchangia katika jambo hili
zito," alisema Sitta.
Alisema
hadi jana mchana alikuwa amepokea majina ya wachangiaji zaidi ya 400
ambao wasingeweza kuchangia kwa siku tatu kama kanuni zinavyoelekeza.
Hata
hivyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi zaidi juu ya jambo hilo alisema
walikuwa wakutane kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi kujadili pamoja na
mambo mengine, suala hilo...
"Kwanza nisiseme sana, maana ndiyo tunaingia kwenye Kamati ya Uongozi, nitafuteni baada ya kikao nitawaelezeni."
Katika
kipindi cha asubuhi, Sitta alisikika akiwataka wajumbe watoe hofu kuhusu
dukuduku la Muungano kwa kuwa watapata fursa ya kuchangia mjadala kwa
wiki nzima bila kufafanua kama itabidi kanuni itenguliwe au la.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 33(7) ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba za mwaka
2014, baada ya taarifa za kamati hizo kuwasilishwa, zitajadiliwa katika
kipindi kisichozidi siku tatu.
Sitta
katika kipindi hicho cha asubuhi, alisema kila siku watachangia wajumbe
50 na kila mmoja atatumia dakika 10 na kwa kuanzia, hiyo jana wajumbe 25
walitarajiwa kupata fursa ya kuchangia.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment