Kuhusu wale Wanajeshi wa Kenya kwenye kampuni za ulinzi Marekani
Kesi
dhidi ya Wanajeshi 27 wa zamani wa Kenya ambao walitoroka jeshini ili
kujiunga na kampuni za ulinzi nchini Marekani imeanza katika kambi ya
kijeshi ya Mtongwe Mombasa.
Unaambiwa Wanajeshi hawa wote walikua wakilitumikia jeshi la Kenya
nchini Iraq, Afghanistan na Kuwait kati ya mwaka 2007 na 2008 na iwapo
watapatikana na hatia wanaweza kufungwa jela kwa miaka miwili bila
kupata nafasi ya kutozwa faini.
Inaaminika kilichowashawishi kuiacha kazi ya Serikali ni malipo makubwa pamoja na maisha yenye unafuu nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment