Milipuko yauwa watu sita Nairobi

Milipuko 
mitatu katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi imesababisha vifo vya watu 6 
na karibu darzeni mbili kujeruhiwa jumatatu usiku katika mtaa mkubwa 
wenye wakazi wengi wa asili ya Kisomali wa Eastleigh.
Mkuu wa 
polisi wa County ya Nairobi Benson Kibue anasema milipuko hiyo ilitokea 
takriban saa moja na nusu usiku na kwa karibu wakati mmoja katika 
migahawa ya Sheraton Café na The New Kwa muzairua Grill.
Kufuatana
 na mmiliki wa Sheraton Café Bw. Patrick Gakuyu watu walikuwa wanatizama
 taarifa ya habari ya saa moja kwenye televisheni wakati aliposikia 
milipuko miwili na umeme kuzimika na kuwa katika kiza. Anasema anadhani 
ni grunetti mbili zilizorushwa ndani ya mgahawa wake.
Jumapili 
usiku karibu na mtaa huo mtu anayedhaniwa ni gaidi aliuwawa alipokuwa 
anatengeneza milipuko yake pamoja na wenzake watatu. Na gruneti moja 
ilipatikana siku hiyo hiyo ya jumapili katika mji wa pwani wa Lamu ndani
 ya kanisa moja.
Usalama umeimarishwa katika miji mikuu ya Kenya na hadi hivi sasa haijulikani aliyehusika na mashambulio ya jumatatu.
(MM)
No comments:
Post a Comment