MRIPUKO WAUWA 71 ABUJA
Hali ya taharuki kufuatia mripuko katika kituo cha basi katika kiunga cha Abuja,Nigeria. (14.04.2014)
Tuhuma
zinaelekezwa dhidi ya kundi la Boko Haram juu ya kwamba hakuna taarifa
ya kudai kuhusika na shambulio hilo kutoka kwa wapiganaji hao wa itikadi
kali za Kiislamu ambapo hasa wamekuwa wakiendesha zaidi harakati zao
kaskazini mashariki mwa Nigeria.Mbali ya watu 71 waliouwawa polisi
imesema watu 124 wamejeruhiwa katika shambulio hilo ambalo ni la kwanza
kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
Kamadori
wa kikosi cha anga Charles Otengbade ambaye ni mkurugenzi wa oporesheni
za msako na uokozi amesema wataalamu wa usalama wanashuku kwamba bomu
hilo limeripuka likiwa ndani ya basi.(MM)
Mabaki ya
maiti za watu zilizorowa damu ilikuwa imetapakaa kila mahala wakati
vikosi vya usalama vikihangaika kudhibiti umma wa watu uliokuwa umezonga
kutaka kujuwa kilichojiri na askari wa zima moto wakilimwagia maji basi
ambalo bado lilikuwa na miili ya abria ilitoketea.
Rais Jonathan aapa kuwashinda Boko Haram
Shambulio
hilo linaonyesha jinsi ilivyo rahisi kwa mji huo mkuu wa Nigeria kuweza
kushambuliwa ambao umejengwa katika miaka ya 1980 kwa kuzingatia umbo
la kijiografia ya nchi kuchukuwa nafasi ya mji wa Lagos kama makao makuu
ya serikali katika nchi hiyo ambayo hivi sasa ndio yenye nguvu kubwa
kabisa za kiuchumi barani Afrika na mzalishaji mkuu wa mafuta.
Rais
Goodluck Jonathan wa Nigeria ameapa kwamba nchi hiyo itaushinda uasi huo
wa kinyama wa kundi la Boko Haram wakati akitembelea eneo kulikotokea
mripuko huo katika kituo cha basi.
Jonathan
akizungumuza kwenye kituo hicho cha basi cha Nyanya kilioko kwenye
viunga vya mji mkuu wa Abuja amesema wamepoteza watu kadhaa na kwamba
suala hilo la Boko Haram ni historia mbaya kabisa inayotokea ndani ya
kipindi cha maendeleo ya nchi hiyo lakini watawashinda Boko Haram na
kwamba suala hilo ni la mpito.
Kuongezeka mashambulizi
Wanamgambo
wa Boko Haram wanopigania kuanzishwa kwa taifa la Kiislamu wamejikita
zaidi katika eneo la mbali la kaskazini mashariki ambapo wamekuwa
wakiendesha harakati zao katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita na
wamekuwa wakizidi kuwalenga raia katika mashambulizi yao ambao
wanawatuhumu kwa kutowa ushirikiano wao kwa serikali na vikosi vya
usalama.
Meja
Yahya Shinku afisa wa zamani katika jeshi la Nigeria anazungumzia kwa
nini mashambulizi hayo yamekuwa yakizagaa kutoka nje ya eneo la
kaskazini mashariki. Amesema "Baadhi ya mashambulio haya yamechochewa
kisiasa na hayawezi kutenganishwa na ukweli kwamba tunaelekea kwenye
uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo kuna watu wana maslahi yao.
Baadhi ya
watu wanaona shambulio hilo sio la kushangaza kwani hali ilikuwa
ikizidi kuwa mbaya na huo ni kama ujumbe kwamba kundi hilo la Boko Haram
bado lingalipo na linaweza kushambulia Abuja wakati wanapotaka na
kusababisha hofu.
Mwandishi : Mohamed Dahman/Reuters/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
CHANZO:DW
No comments:
Post a Comment