TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, September 19, 2014

Waziri Lukuvi achangia Milioni Mbili kwa sare za mgambo 


Katibu wa wa Mbunge wa Jimbo la Isimani Thom Malenga, akizungumza na Wanafunzi wa mafunzo ya mgambo Kata ya Itunundu Jimbo la Isimani

CPL Said Kazumali (Kushoto) mwanajeshi kutoka jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha 42 KJ Songea akizungumza na wanafunzi wa mafunzo ya mgambo mara baada ya kupokea fedha kwa ajili ya sare.


Wanafunzi wa mafunzo ya mgambo Kata ya Itunundu Jimbo la isimani

Na Mathias Canal, Kwanza jamii/Mjengwablog-Iringa
Mbunge wa jimbo la Isimani Mkoani Iringa ambaye pia ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, amechangia shilingi 2,940,000 kwa ajili ya sare za wanafunzi 98 wa mgambo Kata ya Itunundu jimboni humo.
Akizungumza na Kwanza jamii/Mjengwa blog baada ya kukabidhi fedha hizo Katibu wa mbunge, Thom Malenga alisema kuwa fedha hizo zimetolewa na mbunge wa jimbo hilo, kufuatia ombi lililofika ofisi kwake Tarehe 13/09/2014 ya kutaka kupatiwa sare ya mgambo kwa kila mwanafunzi atakayehitimu mafunzo.
"Kwa kuwa mbunge wetu tulimchagua ili kuwatumikia wananchi na wananchi wenyewe ndio sisi,basi amekubali ombi lenu na leo ninawakabidhi fedha hizi kwa ajaili ya kushona sare zenu, nakumbuka wakati nafika jeshini nilihisi kuteswa lakini kadri siku zilivyokwenda niligundua kuwa nilikuwa nafunzwa ukakamavu hivyo hadi leo nimekuwa mkakamavu" Alisema Malenga
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake baada ya kupokea fedha hizo,Aron Sigala ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Itunundu alimpongeza mbunge wa jimbo hilo kutokana na jinsi ambavyo anashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwapatia umeme ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Sigala alisema kuwa mbunge huyo amethamini mafunzo ya mgambo Kata ya Itunundu kwa kujitolea kuwashonea sare wanafunzi wote 98 ambapo kila mtu amechangiwa jumla shilingi 30,000.
Kwa upande wake muuguzi-mkunga wa kijiji cha Itunundu, Hosewa Richard Mgaya alisema kuwa ameamua kujiunga katika mafunzo hayo kwa kuwa ni moja ya mazoezi ya mwili, aliwasisitiza wanawake wenzake kujiunga na mafunzo hayo kwani kufanya mazoezi ni sehemu ya tiba na kuwa mchangamfu.
Alisema kuwa mafunzo wanayoyafanya ni kwa vitendo,mazoezi ya mara kwa mara, matumizi ya silaha,sambamba na kuwa wakakamavu.
Naye CPL Said Kazumali mwanajeshi kutoka jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha 42 KJ Songea, alisema kuwa mafunzo ya mgambo ni sehemu ya kuimarisha afya na ukakamavu lakini pia itawafanya vijana wote washiriki kuwa na upendo na ushirikiano katika kijiji chao.
"Mafunzo ya mgambo yana faida tatu, kwanza ni kuimarisha afya, kuleta faida ya ulinzi katika nchi yako, na kuwalinda wananchi wako" Alisema Kazumali.

No comments:

Post a Comment